TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Jana
tarehe 07/02/2016 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilikuwa na
kikao maalum cha siku moja mjini Dodoma. Kikao hicho kiliongozwa na
Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikao
hicho kilikuwa na kazi ya kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali zilizo
wazi za uongozi ndani ya CCM mikoani na wilayani ambazo uteuzi wake upo
kwenye Mamlaka ya Vikao vya Chama Taifa.
Nafasi
hizi wazi zimetokana na sababu mbalimbali zikiwemo vifo na baadhi ya
viongozi kukihama Chama na kujiunga na vyama vingine. Hivyo, nafasi
zilizofanyiwa uteuzi na wagombea wake ni kama ifuatavyo:-
I. UENYEKITI WA CCM MKOA.
1. ARUSHA
(i) Michael Lekule Laizer
(ii) Emanuel Makongoro Lusenga
(iii) John Pallangyo
2. SHINYANGA
(i) Hassan Ramadhani Mwendapole
(ii) Mbala Kashinje Mlolwa
(iii) Erasto Izengo Kwilasa
3. SINGIDA
(i) Hanje Narumba Barnabas
(ii) Misanga Mohamed Hamis
(iii) Mlata Martha Moses
(iv) Kilimba Juma Hassan
II. UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA NEC
1. NYAMAGANA
(i) DR. Sillinus Elias Nyanda
(ii) Jamal abdul Babu
(iii) Kelebe Bandoma Lutelil
(iv) Patrick Kambarage Nyabugongwe
2. KAHAMA
(i) Pili Yakanuka Izengo
(ii) Paschal Ndibatyo Mayengo
(iii) Sweetbert Charles Nkuba
3. MONDULI
(i) Namelock Edward Sokoine
III. UENYEKITI WA CCM WILAYA
1. MONDULI
(i) Loata Erasto Sanare
2. SUMBAWANGA MJINI
(i) Chami Slegried Mask
(ii) Godfrey Mwimanzi Mwikala
IV. KATIBU WA UCHUMI NA FEDHA MKOA WA KILIMANJARO
(i) Shadrack Amani
(ii) Chata Madata Joseph
(iii) Karia Ahmed Mahamoud
V. KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA ARUSHA
(i) Semmy Rabson Kiondo
(ii) Shaban Omari Mdoe
(iii) Veraikunda Zablon Urio
VI. UENYEKITI WA UVCCM WA MKOA
1. ARUSHA
(i) Erick Edward
(ii) Lengai Loy Thomas
(iii) Mwanzani Omar
2. KILIMANJARO
(i) Amaly T.Mathew
(ii) Frank Lumisha Nkya
(iii) Juma Rahibu Juma
2. SHINYANGA
(i) Mabembela Joseph Elias
(ii) Mipanda kali Dalushi
(iii) Ndasa Jeremiah Damian
(iv) Shigela Reubeen Bernard
Ratiba ya chaguzi hizo itatolewa wiki hii mwishoni.
Kamati
Kuu pia imepokea taarifa ya maandalizi ya uchaguzi wa marudio Zanzibar
na kuridhishwa na maandalizi hayo na kuwatakia kila la kheri Wazanzibar
katika Uchaguzi huo.
Wakati
huo huo, Kamati Kuu imetoa pole kwa Jeshi la Polisi nchini kufuatia
vifo vya Askari Polisi watatu vilivyotokea tarehe 06/02/2016 mjini
Singida kutokana na ajali wakati Askari hao wakitimiza wajibu wao kwenye
maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM. Kamati Kuu inawapa pole
wafiwa wote na kuwaombea majeruhi wote kupona haraka.
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
08/02/2016.
No comments:
Post a Comment