Kamanda wa
Polisi wa Mkoa Katavi Dhahiri Kidavashari akiwa ameshika meno ya Tembo
aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Nzuri Ndizu mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya
Mlele Mkoa wa Katavi ambae alikamatwa juzi akiwa na vipande 8 yenye thamani ya
milioni 120 .
|
Meno ya
Tembo vipande nane (8) vyenye uzito wa kilo 50 ya thamani ya milioni 120 ambayo
ni sawa na tembo hai wanne aliyokamatwa nayo hivi karibuni mtuhumiwa Nzuri
Ndizu Mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi. (Picha na Katavi
yetu blog)
Mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Nzuri Ndizu (44) Mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya
Mlele Mkoani Katavi amekamatwa akiwa na meno ya tembo nane yenye uzito wa
kilogramu 50 yakiwa na thamani ya shilingi milioni 120 ambapo ni sawa na tembo
wanne waliuawa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari
aliwaambia waandishi wa Habari kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa mida ya saa tatu
na nusu.
Kidavashari
alisema mtuhumiwa Ndizu alikamatwa kufuatia misako na oparesheni mbalimbali zinazoendelea
kufanywa na Jeshi la Polisi ikiwa ni kuhakikisha wahalifu wa makosa mbalimbali
wakimemo wawindaji haramu wa wanyama
pori wanakamatwa.
Siku hiyo ya tukio jeshi la polisi lilipata taarifa toka kwa
Raia wema kuwa katika pori la akiba la Lwafe kuna watu wanajihusisha na
biashara haramu ya meno ya Tembo.
Kidavashari
aliendelea kuwaambia waandishi wa Habari baada ya taarifa hizo kupokelewa
ufuatiliaji ulifanyika kwa polisi kufika kwenye eneo hilo na kuweka mtego. ..''Na
walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Nzuri Ndizu akiwa na meno ya Tembo
vipande nane akiwa ameyaficha kwenye pori kwa ajiri ya kusubilia wateja.
Kamanda
Kidavashari alisema mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa
hatua za upelelezi zaidi ilikuendelea kubaini mitandao yote inayojihusisha na
biashara hiyo haramu ya meno ya Tembo na kufikishwa Mahakamani baada ya
upelelezi kukamilika.
|
No comments:
Post a Comment