Miss
Tanzania 1999, Hoyce Temu (wa pili kushoto) akiwa ameambatana
na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa
shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) kushoto Mkuu wa
Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye ( wa pili
kulia), Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa (kulia) pamoja
na mpiga picha wa kipindi cha Mimi na Tanzania, Geofrey Magawa a.k.a KIM
(kushoto) wakiwasili Desemba 31, 2015 kwenye makazi ya wazee na watu
wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es
Salaam.
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Miss Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu amemaliza
mwaka 2015 kwa kutembelea kituo Nunge ambacho ni makazi ya wazee na
walemavu wasiojiweza kilichopo Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es
Salaam.
Hoyce
ambaye amekuwa akisaidia watu wa aina mbalimbali wenye matatizo ikiwa
ni kama moja ya kazi wanazofanya mamiss kwa jamii pia kupitia kipindi
chake cha Mimi na Tanzania ambacho kimekuwa kikisaidia watu mbalimbali
na katika halfa hiyo aliongozana na watu wake wa karibu ikiwepo kamati
ya Miss Tanzania.
Katika
halfa hiyo iliyodhaminiwa na Malaika Beach, Hoyce baada ya kuwasili
kituoni hapo yeye na timu nzima aliyoongozana nayo walifanya shughuli za
kijamii katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika
makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza waliopo kituoni kwa kupulizia
dawa za kuulia wadudu katika nyumba zao, kugawa dawa za mbu, maji, juice
na biskuti na baadae wakapata chakula cha pamoja na wazee na walemavu
wasiojiweza.
Akizungumzia
halfa hiyo ya kufunga mwaka, Hoyce Temu alisema kumekuwepo na
kusahaulika kwa makundi ya watu wasiojiweza na jinsi muda unavyokwenda
wanazidi kusahaulika na jamii inayowazunguka.
Alisema
yeye kama Miss Tanzania ana wajibu wa kujitoa kuwasaidia watu wa aina
hiyo na amekuwa akifanya maeneo mengi kwa kujumuika nao kwa kuwapa
msaada na kuwafariji kwani nao wana thamani kama binadamu wengine.
"Kadri
inavyokwenda kumalizika karne ya 21 kunazidi kuongezeka kwa makundi ya
wasiojiweza na mimi kama Miss Tanzania nimeamua kujitoa kwa kusaidia
makundi haya kwani ni wajibu wetu na tukumbuke na sisi tunaelekea huko," alisema Hoyce.
Aidha
Hoyce alitoa ushauri kwa mamiss wenzake kuwa wanatakiwa kuisaidia jamii
kwa kutumia fursa walizonazo mbele ya jamii kwa kutoa misaada kwa
makundi ya aina mbalimbali.
Alisema
kazi ya kusaidia jamii siyo ya serikali pekee na wao kama mamiss na
watu wenye uwezo kwa ujumla wana wajibu wa kusaidia na sio kutazama
mijini pekee kutokana na kundi kubwa la wasiojiweza kuwa vijijini.
"Sio
swala la serikali pekee ... ukichaguliwa kuwa mrembo unakuwa na malengo
ambayo umeyaweka hivyo watumie umaarufu, sura zao na sauti kufikia watu
wa aina mbalimbali ambao wanahitaji msaada, "
Na sio wazee pekee, 65% ya nchi yetu ni vijana na 20% wanajihusisha na
kutumia madawa ya aina mbalimbali hivyo wanaweza kuwatembelea na kutoa
elimu juu ya athari za utumiaji wa madawa hayo," alisema Hoyce.
Mdau Matukio Chuma na Dada yake Hoyce Temu, Bi. Edith wakifurahi jambo wakati walipowasili kwenye kituo cha Nunge.
Nae
Mkurugenzi wa Lino International Agency, ambayo ndiyo waandaji wa
shindano la Miss Tanzania, Hashimu Lundenga alimtaja Hoyce kama Miss
bora kuwahi kutokea tangu walipoanzisha shindano la Miss Tanzania mwaka
1994.
Alisema
mamiss wengi wamekuwa wakiisaidia jamii lakini Hoyce amekuwa akijitoa
zaidi kuliko wengine na kufanya shindano hilo kuonekana kuwa na faida
mbele ya jamii.
"Naomba
niseme ukweli Hoyce anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa haijawahi kutokea
miss aliyejitoa kusaidia jamii kama yeye na wapo wengine wanasaidia ila
Hoyce amekuwa mstari wa mbele kwa hilo tunampongeza na tunamwomba azidi
kuwa hivyo," alisema Lundenga.
Kwa
upande wa Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi amemshukuru
Hoyce kwa upendo amekuwa nao kwa kituo hicho ambacho awali aliwahi
kukitembelea 2006 akiwa na marehemu Amina Chifupa na kumtaka kuzidi kuwa
na moyo huo kwa jamii inayomzunguka.
Mgedzi
pia alizungumzia changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na kutokuwepo
kwa uzio hivyo kutokuwa na hali ya usalama, kuvamiwa kwa eneo hilo na
wananchi ambalo lina hekali 50.8 na tayari asilimia 50 imevamiwa na
tayari taarifa ipo wizarani na wanashughulikia na zingine ndogo ndogo
Hoyce akiahidi kuwasaidia.
Nae
mmoja wa washiriki aliyeongozana na Hoyce, Tausi Mwenda alisema kuwa
amejifunza mambo mengi kupitia halfa hiyo aliyoifanya Hoyce na
kuwashauri watu wa aina mbalimbali kuwa na moyo wa kujitoa kusaidia
jamii kama anavyofanya Hoyce.
Baadhi
ya wadau waliombatana na Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (hayupo
pichani) akiwemo Bi. Tausi Mwenda Mke wa aliyekuwa Meya wa Kinondoni,
Yusuph Mwenda, (katikati) wakifurahi jambo walipowasili kwenye kituo cha
Nunge, makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo
Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Miss
Tanzania 1999, Hoyce Temu akimkumbatia rafiki yake wa siku nyingi mmoja
wa wazee wenye ulemavu uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija
(66), wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu
wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31,
2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na
kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss
Tanzania 1999, Hoyce Temu akiendelea kufurahi na rafiki yake wa siku
nyingi mmoja wa wazee wenye ulemavu uliotokana na ugonjwa wa ukoma,
Mganga Shija (66), wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye
ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam
Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka
2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss
Tanzania 1999, Hoyce Temu akitazama jicho la upande wa kulia
linalomsumbua mzee Mganga Shija (66), ambaye aliomba kusaidiwa matibabu
CCBRT wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu
wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31,
2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na
kukaribisha mwaka mpya 2016.
Afisa
Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi (kushoto) akitoa taarifa fupi
ya maendeleo ya kituo hicho kwa Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu
aliyeambatana na Kamati ya Miss Tanzania kwenye ziara hiyo.
Mkurugenzi
wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss
Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza jambo na Afisa Mfawidhi wa kituo
cha Nunge, Ojuku Mgedzi.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiserebuka na mmoja wa wazee wanaoishi kwenye makazi ya Nunge kituoni hapo.
Bi.
Edith (kulia) ambaye ni Dada wa Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiteta
jambo Bi. Tausi Mwenda mke wa aliyekuwa Meya wa Kinondoni, Yusuph
Mwenda kabla ya kuelekea kwenye zoezi la upigaji wa dawa.
Baadhi ya nyumbani za makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Miss
Tanzania 1999, Hoyce Temu (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Lino
International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania,
Hashim Lundenga (kulia) na Tausi Mwenda (kushoto) wakichanganya dawa ya
kuulia wadudu tayari kwa kupulizwa katika nyumba kwenye makazi ya wazee
na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar
es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii
kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss
Tanzania 1999, Hoyce Temu akisaidia kupuliza dawa ya kuuwa wadudu
katika moja ya nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu
wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Desemba 31,
2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na
kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss
Tanzania 1999, Hoyce Temu akizungumza na mmoja wa wazee (jina lake
halikupatikana) kabla ya kumpigia dawa ya kuua wadudu nyumbani
kwake wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu
wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31,
2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na
kukaribisha mwaka mpya 2016.
Dada
yake Hoyce Temu, Bi. Edith akishiriki kuondoa vyakula vyombo ili
kuruhusu zoezi la upigaji wa dawa ya kuulia wadudu kwenye makazi ya
wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni,
jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya
kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss
Tanzania 1999, Hoyce Temu akigawa chakula kwa watoto katika makazi ya
wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza iliyopo Nunge, Kigamboni, jijini
Dar es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya
kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.Kwa matukio zaidi bofya hapa
No comments:
Post a Comment