SHEREHE ZA 52 MAPINDUZI YA ZANZIBAR:-Zaanza rasmi kwa usafi wa Mazingira. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 03, 2016

SHEREHE ZA 52 MAPINDUZI YA ZANZIBAR:-Zaanza rasmi kwa usafi wa Mazingira.

IMG_3011
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizoa taka katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

IMG_3016
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akibeba taka katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
DSC_8792
Baahi ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wakitandaza kifusi kwa kukiweka sawa katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
IMG_3034
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B.Unguja Ayoub Maohammed Mahmoud wakati zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.Picha na Ikulu.
1 (2)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifanya mahojiano na waandishi wa Habari leo baada ya kumalizika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akishiriki na Wananchi, Vikundi ya vya usafi wa mazingira pamoja na Vikosi vya Ulinzi kwenye usafi wa mazingira hapo Kwahani Uwanja wa Farasi ikiwa ni kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Baadhi ya wapiganaji wa Vikosi vya ulinzi wakishiriki zoezi la usafi wa mazingira katika Mtaa wa Kwahani Uwanja wa Farasi kuanza kwa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 52. Picha na – OMPR – ZNZ.
Kazi za usafi wa mazingira kwenye maeneo tofauti Nchini katika kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeonekana kuitikiwa vyema na Wananchi walio wengi pamoja na vikosi vya ulinzi hapa Nchini.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alijumuika na Wananchi hao kwa kazi za usafishaji wa Mtaro wa maji machafu unaokusanya maji kutokea mitaa ya Muembe Njugu, Kwahani, Kariakoo, Kilimani na Kumalizikia Pwani ya Kilimani.

Akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhandisi wa Baraza la Manispaa Zanzibar Nd. Mzee Khamis alisema Baraza la Manispaa limeanzisha mradi maalum wa usafi wa mazingira katika Manispaa ya Zanzibar kwa kuwashirikisha moja kwa Wananchi kwenye Mitaa yao.
Mhandisi Mzee alisema hatua hiyo itatoa fursa pana kwa kila mwananchi kuona kwamba suala la usafi wa mazingira ambalo linapaswa kuwa la kudumu linaigusa Jamii moja kwa moja badala ya kufikiria kuwa jukumu hilo ni la Baraza la Manispaa pekee.

Akizungumza na washiriki wa zoezi hilo la usafi wa mazingira kwa ajili ya kuanza kwa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 52 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwapongeza Wananchi pamoja na Vikosi vya ulinzi kwa ushiriki wao wa usafi wa mazingira.

Katika kazi hiyo ya usafi wa mazingira kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi zawadi ya vifaa tofauti vya usafi wa mazingira kwa Kikundi cha usafi wa Mazingira cha Kilimani City.

Vifaa hivyo vyenye Thamani ya Shilingi Laki Saba vimetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Idara yake ya Mazingira ikiwa ni muendelezo wa utaratibu iliyojipangia wa kutoa zawadi za vifaa kila mwaka kwa Vikundi vilivyoonyesha juhudi katika kushiriki kwenye usafi wa mazingira maeneo mbali mbali Nchini.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad