NATOA TAHADHARI :-Wahusika wa Barabara ..Mnasubiri Maafa Hapa Mto Kasisi-Sikonge Road-Tabora.?? - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 17, 2016

NATOA TAHADHARI :-Wahusika wa Barabara ..Mnasubiri Maafa Hapa Mto Kasisi-Sikonge Road-Tabora.??

Mto Kasisi ni mto wa msimu wa mvua, ambao ni mpaka wa Wilaya ya Uyui (Tabora vijijini) na Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

 Daraja hili ambalo unaliona kwenye picha hizo, hapa ndipo yanapita Magari ya mizigo na Mabasi ya Abiria yanayokwenda Sikonge, Mpanda ( Katavi ) na Mbeya.

  Pia yanayotoka mkoani Mbeya, Katavi, Rukwa n.k kuelekea Tabora, Shinyanga, Mwanza n.k yanapita juu ya daraja hili hatari.



……’’Sisi tunaopita hapa kwa baiskeli, pikipiki na miguu, ndio tunaona vizuri hatari inayowakabiri wapitaji wa Magari kama wahusika hawatachukua hatua za haraka bila kuchelewa..’’…..

Mto huu kwa sasa umejaa maji tofauti na mwaka jana 2015,ambapo ulikuwa na maji machache kiasi. Udongo katika daraja umeanza kubomolewa na kasi ya maji! Wahusika ( viongozi wa serikali ) wanayaona haya, maana njia yao ni  hii!

Jambo la ajabu hapa hata alama za Barabara za kuonesha uwepo wa daraja hakuna!

Wahusika wasipochukua hatua, TCRA mjiandae
kunidaka nikiripoti tukio.

MWISHO WA KUTOA TAHADHARI!!
Na:- David Carol –TABORA.




Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad