MAPINDUZI CUP 2016:-Kipigo cha Mtibwa Sugar chawavua Simba SC Ubingwa wa Kombe ambalo walilitwaa Mwaka Jana 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 10, 2016

MAPINDUZI CUP 2016:-Kipigo cha Mtibwa Sugar chawavua Simba SC Ubingwa wa Kombe ambalo walilitwaa Mwaka Jana 2015.


Ibrahim Rajab Jeba (kulia) akishangilia na wenzake baada ya kufunga.

Simba SC imevuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, baada ya kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Nusu Fainali uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar jioni ya leo January 10, 2016.

Shujaa wa Mtibwa Sugar FC leo alikuwa ni kiungo Ibrahim Rajab ‘Jeba’ aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 45 akimalizia mpira uliopanguliwa na kipa Peter Manyika baada ya shuti la mshambuliaji Hussein Javu anayecheza kwa mkopo kutoka Yanga SC.

Kipa Said Mohammed wa Mtibwa Sugar (kulia) akiwa amedaka mpira wa Mwinyi Kazimoto aliyeruka juu.

Mussa Mgosi wa Simba SC (kulia) akimtoka Shizza Kichuya wa Mtibwa Sugar.

Kipigo hiki kimewavua Simba Ubingwa wa Kombe hili ambalo walilitwaa Mwaka Jana walipoitoa Mtibwa Sugar kwa Penati 4-3 kwenye Fainali.

Mtibwa Sugar sasa wametinga Fainali na watacheza na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine itakayochezwa Usiku huu kati ya Yanga na URA ya Uganda.

Mapinduzi Cup

Mabingwa waliopita

-2007 Yanga SC

-2008 Simba SC

-2009 Miembeni

-2010 Mtibwa Sugar

-2011 Simba SC

-2012 Azam FC

-2013 Azam FC

-2014 Simba

-2015 ??????

Mfungaji wa bao pekee la Mtibwa, Ibrahim Jeba (kushoto) akimtoka beki wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala'Picha kwa hisani ya BIN ZUBEIRY.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad