TAZAMA PICHA:-Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Wachezaji wa Ndani 2015..Mbwana Ally Samata alivyopokelewa Tanzania . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 10, 2016

TAZAMA PICHA:-Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Wachezaji wa Ndani 2015..Mbwana Ally Samata alivyopokelewa Tanzania .

Mbwana Samatta akipata picha ya pamoja na Waziri Mh.Nape Nnauye. Mwanasoka huyo aliwasili Ijumaa January 08,2016,Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam akitokea Abuja, Nigeria katika hafla ya utoaji tuzo kwa mwanamichezo bora.

PICHA NA MICHUZI JR-MMG.

Mbwana Samatta ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Anayecheza Afrika katika sherehe zilizofanyika usiku wa Alhamisi ukumbi wa mikutano wa Kimataifa mjini Abuja.
Samatta alipata pointi 127, mbele ya mchezaji mwenzake wa TP Mazembe, kipa Robert Muteba Kidiaba wa DRC, aliyepata pointi 88, wakati mshambuliaji wa Etoile du Sahel ya Tunisia na timu ya taifa ya Algeria, Baghdad Bounedjah amepata pointi 63.
Mafanikio ya Samatta anayeweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa ukanda w Afrika Mashariki na Kati kushinda tuzo kubwa ya Afrika, yanakuja baada ya kuiwezesha Mazembe kutwaa taji la tano la Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akiibuka mfungaji bora kwa mabao yake nane. 

Aidha, Samatta sasa ndiye anaweza kuitwa Mchezaji Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania – bada ya miaka mingi ya kutokuwa na uhakika wa nani apewe sifa hiyo.

Samatta alijiunga na Mazembe mwaka 2011 akitokea Simba SC aliyoichezea kwa msimu mmoja akitokea African Lyon iliyomtoa Mbagala Market, ambayo ilimuibua Kumbagulile FC ya kwao, Mbagala.
Baadae akawasili viwanja vya Escape One akiwa ameambatana na Waziri Nape Nnauye tayari kwa kukamilisha ratiba nyingine,pia alipata selfie na washabiki wa soka kama uonavyo pichani.
Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba sambamba na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape na wadau wengine wa soka wakijumuika kwa pamoja kumpongeza Samatta. PICHA NA MICHUZI JR-MMG.

Msafara wa magari uliokuwa umembeba Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Wachezaji wa Ndani 2015, Mbwana Samata,ulionaswa na Camera ya Globu ya jamii maeneo ya Morocco jana,January 09,2016 jioni ukitokea hoteli ya Kempinsk baada ya kuzungumza na vyombo vya habari,Msafara huo akiwemo Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye ulipita maeneo kadhaa ya jiji la Dar na kukomea katika kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar,ambako alikutana na kupongezwa na Wadau mbalimbali wa tasnia ya Michezo.Mwanasoka huyo aliwasili juzi,Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam akitokea Abuja, Nigeria katika hafla ya utoaji tuzo kwa
mwanamichezo bora.

PICHA NA MICHUZI JR-MMG.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad