Viongozi wa
Kitongoji cha Kasalazi, kilichoko katika Kijiji cha Kanyara, Kata ya Bulyaheke,
wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza, wanadaiwa kuwachapa fimbo hadharani
wanawake wanaovaa nguo fupi zinazoonyesha baadhi ya sehemu zao za siri.
Pia, viongozi
hao wanadaiwa kuwatoza faini ya Sh 20, 000 wanawake wanaokutwa na nguo hizo
kama njia ya kuwafanya wasiendelee kuvaa nguo hizo.
Mmoja wa
wasichana waliowahi kuchapwa na viongozi hao aliyejitambulisha kwa jina la
Juliana Mafuru, alichapwa fimbo baada ya kufika kijijini hapo kwa lengo la
kununua dagaa.
“Cha
kushangaza ni kwamba, baada ya kufika katika kitongoji hicho, mgambo
walinikamata na kunichalaza bakora mbele za watu nje ya boti niliyokuwa
nimepanda.
“Pia
waliamuru nivue suruali niliyokuwa nimeivaa na kuanza kuichana chana nyembe.
“Wakati
wananifanyia hivyo, walitokea wasamalia wema ambao walinipatia shuka la kimasai
ili niweze kujisitili, yaani waliniabisha kweli.
“Baadaye,
walinipeleka kwenye ofisi ya kitongiji hicho na walinitoza faini ya shilingi
20,000, kisha wakaniachia,” alisema Juliana.
Nao wakazi
wa kijiji hicho, Lafael Bitulo na Mariamu Chacha, walisema mwenyekiti wa
kitongiji hicho na katibu wake, ndiyo vinara wa tabia hiyo kwa kuwa wamekuwa
wakinufaika nayo.
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Andrea Mkama, alikiri kuwachapa fimbo
wanawake wanaovaa nguo fupi na zinazobana kwa mavazi wanayovaa ni ya
udharirishaji.
Naye
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kanyara, Lazoro Mgonzo, alithibitisha
wanawake kuchapwa fimbo ingawa alisema ni kitendo cha udharirishaji.
Mkuu wa
Wilaya Sengerema, Zainabu Terack alipoulizwa juu ya tukio hilo, alisema hana
taarifa ingawa aliahidi kulifuatilia.
Source:- Mpekuzi
blog.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment