Watanzania
leo,January 11, 2016, wanaanza kufaidi elimu bure kufuatia kufunguliwa kwa
shule za umma huku Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce
Ndalichako, akisema fedha zimeshafika kwa kila shule.
Aidha, Prof.
Ndalichako amewataka wamiliki wa shule binafsi kujitathmini.
Itakumbukwa
kuwa serikali ilipoanzisha Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi na Sekonari
mwaka 2000, lengo lilikuwa ni kutoa ruzuku ya Sh.10,000 kwa kila mwanafunzi wa
shule ya msingi na Sh. 25,000 kwa kila mwanafunzi wa sekondari kwa mwaka.
Ruzuku hiyo
inalenga kugharimia ununuzi wa vitabu vya kiada na ziada, vifaa vya kufundishia
zikiwamo chaki, madaftari, kalamu za risasi na wino, karatasi za kufanyia
mitihani, ukarabati miundombinu ya shule na shughui za utawala.
Juzi, Prof.
Ndalichako alisema kuwa fedha za ruzuku
kwa wanafunzi shule za msingi na sekondari, zimeshapelekwa, lengo likiwa ni
kuhakikisha leo wanafunzi wanaanza masomo.
“Fedha hizi
zitakuwa zikitolewa kwa awamu, kwa hiyo zilizokwenda ni awamu ya kwanza tu,”
Alisema Profesa Ndalichako
Prof.
Ndalichako alisema ili kuhakikisha fedha zote zinazotolewa zinafika kwa walengwa,
watashirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), kuhakikisha zinawafikia walengwa.
Alisema moja
ya njia ya kufikia lengo hilo ni kutoa fedha hizo kwa awamu na kuhimiza
uaminifu kwa watu wote wanaohusika.
Ada Elekezi
Kwa Shule Binafsi.
Akizungumzia
ada elekezi, alisema suala hilo ameona ni vyema lifanyiwe utafiti kwa kila
shule kufafanua matumizi ya fedha wanazotoza na kuwa na baada ya kukubaliana
ada elekezi, watakaokiuka watakabidhiwa kwa Mamlaka ya Mapato (TRA), ili
watozwe kodi.
“Hili suala
nimelikuta na nikaona ni vyema tufanye utafiti kidogo. Sasa hivi shule nyingi
tayari zina viwango vya ada na vina tofauti kubwa tu. Kwa kuanzia, nimeona
tuanze na ada zilizopo, tayari nimeshaelekeza na kazi imeanza kwa kutaka wamiliki
wa shule watoe `justification’ (hoja za kuhalalisha) ada wanazotoza,” alisema na kuongeza:
“Nimeona
kuna umuhimu wa kushirikisha hawa watu na kuwasikiliza, ndiyo maana tukasema
kwanza wao watupatie hayo maelezo. Mtu aseme labda anatoza Sh. milioni tano,
atuambie ana walimu wangapi, mishahara yao Sh. ngapi? Gharama za umeme ni Sh. ngapi?
"Akisema
gharama za chakula na sisi tunazijua, tutaangalia hata kama anawapa watoto
soseji, tutaangalia bei na kadhalika, tunachotaka kwanza tutafute uhalisia wa
hizo ada.
“Najua kuna
baadhi ya maeneo tutakosa uhalisia maana mwingine anatoza bei ya umeme labda kila
mwanafunzi Sh. 20,000, kama ana
wanafunzi 500, jumla yake itakuwa Sh. ngapi? Tutamwambia atupe bili ya umeme
tuthibitishe,” alisema Pro. Ndalichako.
Alisema
wameamua kufanya hivyo kwa kuwa shule binafsi zina mazingira tofauti na hivyo
ni vigumu kuwa na ada elekezi moja ambayo kweli inatekelezeka.
“Ada elezi
haiwezi kuwa sawa kwa sababu shule zina viwango tofauti na walimu aina tofauti.
Hata maeneo zilipo, ni tofauti, pia kuna huduma tofauti zinazotolewa na shule
hizi.
Kila shule
ikitoa mchanganuo, tujua kilichopo, tukiwa na data (takwimu) itatusaidia kujua
mengi na sisi kujipanga vizuri, hata vyakula wanavyotoa tutaviangalia na
kuvihakiki, usije kutoza Sh.15,000 kwa
chakula kwa siku halafu ukampa mtoto ugali na maharage,” alisema.
Alisema
pamoja na mambo mengine, vitu hivyo vitathibitishwa na wakaguzi wa shule na
pale inapobidi wazazi watashirikishwa ili kupata uhalisia.
“Tutachukua
muda, lakini tutakuja na majibu ambayo Watanzania wote watakubali kwa sababu
sasa hivi wapo ambao hawapo na sisi wizara, hatutaki kumwambia mtu anayetoa
kompyuta, na vitu vingine muhimu kwa mwanafunzi aache.
"Lazima
tushirikiane nao ili hata kwenye utekelezaji tufanikiwe, ambacho hatutaki ni
shule kutumia sana wanafunzi kama sehemu ya kipato na tukiweka ada elekezi wale
watakaotoza zaidi, tutawapeleka TRA wawatoze kodi kwa sababu hawa wanafanya
biashara, wanazalisha,” alisema Prof. Ndalichako.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment