Dada Joyce
akiwa wodini MOI -Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Dar es Salaam.
|
Ankal akiwa
wodini kumtembelea dada Joyce.
|
Dada Joyce
alipowasili Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki iliyopita.
Ndugu Wasamaria Wema,
Tunapenda kutumia fursa hii kuwashirikisha tena habari
ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Rishard Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye wa
miaka 4, na miguu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya.
Dada huyu
mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na
huyo mwanaye wa miaka 4.
Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana wa 2014 dada
huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo dereva hakusimama kumsaidia.
Ila
kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Mbeya ambako alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu, kwa kukosekana
nyenzo pamoja na pesa za kumfanyia uchunguzi.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce
amevunjika miguu yote miwili, hivyo akahamishiwa katika hospitali ya
Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa tena
Mbeya baada ya kukosa pesa za vipimo na matibabu.
Hadi Msamaria mwema na Mpiganaji Deo Kakuru
anakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake ambaye ni mlezi
wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wake wote wawili kufariki
dunia.
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo
kitandani kwa msaada wa mwanaye huyp na bibi yake. Inasikitisha.
Hivyo Deo Kakuru, kwa msaada mkuwa wa michango ya
Wasamaria Wema, amefanikiwa kumsafirisha dada Joyce kwa Fast Jet kutoka
Hospitali ya Rufaa ya Mbeya hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo
cha MOI jijini Dar es salaam ambako alipokelewa na kulazwa katika jengo jipya
liitwalo Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu wodi namba 2.
------------------------------
UPDATES:
Baada ya Deo Kakuru kuweka mitandano tatizo la dad Joyce,
Wasamaria Wema kadhaa wakajitokeza kumsaidia. Hatuna uhakika kwamba wote
wangependa majina yao yawekwe hadharani, Ila tunapenda hadi sasa kukiri
upokeaji wa Tshs:-
1. 505,000/-
2. 50,000/-
3.100,270/-
4. 10,000/-
5. 100,000/-
6. 500,000/- (ahadi ya uhakika)
7. 500,000/- (Michuzi Media Group)
7. 800,000/- (Kulipia gharama za vipimo vya CT Scan Regency
Hospital mgonjwa atapofikishwa Dar es salaam).
Hivyo ndiyo kusema jumla ya Tshs. 2,565,270/- tayari zilikusanywa kumsaidia dada yetu huyu anayeteseka. Kwa niaba ya mgonjwa tunashukuru sana kwa msaada huo, hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mola mzidishiwe pale mlipopungukiwa. KUTOA NI MOYO. Aidha, kwa kiasi kilichopatikana tayari dada Joyce ameshafanyiwa vipimo vya MRI Alhamisi iliyopita na hivi sasa yanasubiriwa majibu siku ya Jumatatu ambapo baadaye Jopo la Madaktari Bingwa litaka na kuamua nini kifanyike kimatibabu.
Tunashukuru madaktari na watumishi wote wa MOI kwa kuhitimisha
hilo, nasi tunaendelea kuwaomba waendelee na huduma hiyo hadi dada Joyce
atapopata matibabu.
Vile vile tunamshukuru sana Msamaria Mwema Mama Rozi aliyejitolea
kumhudumia dada Joyce pale wodini ambako mama yake mzazi amelazwa na ana
matatizo karibu sawa na ya dada yetu.
Bila kuchoka mama Rozi amekuwa akimletea
chakula na vinywaji dada Joyce kila siku na kumfanyia huduma za usafi kila
siku. Ubarikiwe sana Mama Rozi.
Shukurani pia ziwaendee wasamaria wema wengine pamoja na wadau
ambao baada ya kuguswa na matatizo ya dada Joyce wamekuwa wakimtembelea hapo
wodini na kumfariji. Asanteni sana.
Wito wetu tunaomba tuendelee kumsaidia kwa hali na mali dada Joyce kwani mara baada ya majibu ya vipimo yatapotoka Jumatatu, ni dhahiri kutakuwa na mahitaji zaidi katika matibabu yake. Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal anaendelea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha MOI.
Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa
email issamichuzi@gmail.com
Mratibu mwenza Deo Kakuru naye anaendelea kusaidia kwa kumtunza
bibi yake Joyce na mwanae mwenye umri wa miaka 4 huko Mbeya.
Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema
+255769 512 420
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp . |
No comments:
Post a Comment