Mbunge
Mteule wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa na Aliyekuwa Mgombea Urais wa
Chadema, Edward Lowassa
MGOMBEA
Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Arusha Mjini,
Godblees Lema ameibuka mshindi na kutangazwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha vyama
vitano vya siasa, Lema amepata kura 68,848 kati ya kura 104,353 zilizopigwa
sawa na asilimia 65.9 akifuatiwa na Mgombea wa CCM, Philemon Mollel aliyepata
kura 35.907 sawa na asilimia 34.4.
Wagombea
wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni Navo Mollel wa ACT-Maendeleo
aliyepata kura 342 sawa na asilimia 03, Zuberi Mwinyi wa CUF aliyepata kura
106, sawa na asilimia 0.1, na Makama Rashidi wa NRA aliyepata kura 43 sawa na
asilimia 0.04.
Kwa mujibu
wa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Juma Iddy, jimbo la Arusha wapiga kura
walioandikishwa ni 317.814, na waliojtokeza kupiga kura ni 105,800 sawa na
asilimia 32.83 na kura halali ni 104,353.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp . |
Monday, December 14, 2015
UCHAGUZI JIMBONI:-Ni Lema tena Arusha Mjini.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment