Meza
kuu,wa kwanza kulia ni Meneja wa redio PANGANI FM Maimuna Msangi, wa
pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA ambalo limeratibu
tamasha hilo VERA PIEROTH,wa tatu ni Kaimu mgeni Rasmi ambaye pia ni
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya PANGANI Bi Patricia, na wanne ni
Mratibu wa masuala ya UKIMWI wilaya ya PANGANI.
Mkurugenzi
wa shirika la UZIKWASA, VERA PIEROTH akizungumza jambo wakati wa
kuwakaribisha wananchi wa PANGANI katika tamasha hilo.
Na Mwandishi wetu
Shirika
lisilo la kiserikali Wilayani Pangani la UZIKWASA linalojishughulisha
na kuziwezesha kamati za kudhibiti Ukimwi, VMACK limezawadia kamati bora
za kudhibiti ukimwi Wilayani humo.
Sherehe hizo zimefanyika sanjari na kuwazawadia kijana bora mfano wa kuigwa na mama bora mfano wa kuigwa.
Katika
sherehe zilizofanyika kijiji cha Jaira,K ata ya Madanga wilayani
Pangani na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wananchi na viongozi
kutoka halmashauri ya Wilaya ya Pangani mgeni rasmi alikuwa Kaimu Afisa
Maendeleo Wilaya ya Pangani, Bi.Patricia Kinyange.
Akizungumza
katika hadhara hiyo Bi. Kinyange amelipongeza shirika hilo kwa
kuzijengea uwezo kamati hizo ambazo zinafanya kazi kubwa kwa jamii.
“Kwa
kweli shirika la UZIKWASA nawapongeza sana, mnafanya kazi kubwa kwenye
jamii ya Pangani na kwakweli watu wa Pangani wanapaswa kujivunia uwepo
wenu. Nimeshangaa kuona mambo makubwa yanayofanywa na kamati kutokana na
elimu mnayowapatia,mnastahili pongezi kubwa”alisema Bi.Kinyange.
“Mfano
mzuri mimi ARUSHA nilipokua nafanya kazi, kamati zipo lakini kwakweli
wamelala,unakuta kamati inakutana mara mbili kwa mwaka mzima,lakini huku
ni zaidi ya mara kumi,kwakweli nimeshangaa sana,nyinyi ni shirika
ambalo linafaa kuigwa,lakini wanakamati niwaombee mzidishe juhudi
msiwaangushe wanauzikwasa na sisi kama halmashauri tutajitahidi
kushirikiana kwa karibu kabisha na UZIKWASA ili kuendeleza juhudi hizi.”
Katika
hatua nyingine mgeni huyo rasmi amempongeza kijana aliyeibuka mshindi
katika shindano la kijana bora mfano wa kuigwa na kumtaka kuendeleza
juhudi zake na kwamba Halmashauri watamtumia kama darasa kwa ajili ya
vijana wengine kujifunza kutoka kwake.
Kwa
upande wao kamati iliyoibuka mshindi kwa mwaka wa tatu mfululizo kutoka
katika kijiji cha Mseko wamesema umoja na mshikamano ndio nguzo pekee
ya ushindi wao,na kwamba shukrani pekee zinapaswa kwenda kwa UZIKWASA
kwa mafunzo na ufuatiliaji wao kwani ndio vilivyowafanya kutekeleza
mipango waliojiwekea kama wanakamati hadi kuibuka washindi.
‘Naweza
kusema kamati yetu imejitoa sana,wanakamati wanatumia muda wao mwingi
wa ziada katika kuhakikisha tunatekeleza mipango tuliojiwekea,lakini pia
msukumo mkubwa ni kutoka UZIKWASA kwakweli tunawashukuru sana”Alisema
Afisa mtendaji mseko.
Kwa
upande wake Mratibu wa shughuli hizo kutoka shirika la UZIKWASA ambaye
pia ni Afisa wa mradi wa jinsia na uongozi wenye mabadiliko, Bi.Salvata
Kalanga amesema haikuwa kazi rahisi kuzipata kamati bora 8,kutokana na
ushindani mkubwa uliokuwepo kwa washiriki 15,lakini wanashukuru kumpata
mshindi ambaye wanaamini anastahili kutokana na kazi waliyoifanya.
Katika
sherehe hizo,mshindi wa kwanza amepata zawadi ya ngao,pamoja na fedha
taslimu shilingi laki sita,mshindi wa pili alipata laki 4 na nusu,na
mshindi wa tatu alipata shilingi laki 4.
Sherehe
ya kuzizawadia kamati bora za kudhibiti UKIMWI hufanyika kila mwaka
chini ya shirika la UZIKWASA,lengo ni kuzipa motisha kamati hizo ili
zifanye vizuri zaidi.
Mashindano
haya na tamasha hili husimamiwa na kuwezeshwa na Asasi ya UZIKWASA
Pangani kwa lengo na Kuamsha hamasa, kuchochea, kutafakari na kujifunza
na kujenga uwajibikaji miongoni mwa vijana, akinamama na Kamati za
Kudhibiti UKIMWI jinsia na uongozi za vijiji.
Mashindano
haya huanza baada ya UZIKWASA kuwezesha kamati hizi kwa kuzijengea
uwezo na baadae maafisa wa UZIKWASA kuzitembelea kamati hizo na
makundi yaliyotajwa na kupima utekelezaji wake kwa kuzingatia vigezo
vilivyowekwa na kukubaliwa na wadau hao.
Kamati,
vijana, na akina mama walioanishwa kufanya vizuri hutembelewa na kamati
nyingine kuweza kujifunza kwa pamoja na kujirudhisha kwa utekelezaji wa
kamati hizo.
Pia kwa vijana na wakinamama hutembeleana na kupeana
taarifa za utekelezaji na kujifunza kwa pamoja. Kamatai hizo na hao
vijana na akinamama huchujwa na kubaki wachache ambao wanatekeleza
vizuri zaidi.
Baada
ya zoezi hilo la kutembeleana walioanishwa huitwa Pangani na
kukutanishwa na waamuzi ambao huwasikiliza na kuchambua washindi.
Mwaka
2015 kamati 12 zilichaguliwa kuingia kwenye ushindani huo ambazo ni
Mseko, Mwembeni, mkwajuni, mbulizaga, Bweni, mzambarauni, Mtonga,
Mikocheni, Langoni,Tungamaa, Sange na Jaira.
Akina
mama bora waliongia sita bora kati ya 33 ni kutoka Masaika, Kwa kibuyu,
Stahabu, Mwembeni, Mtonga na Langoni. (watatu watazawadiwa)
Vijana bora waliongia sita bora kati ya 33 ni kutoka Msaraza, Kimanga, Mikocheni, Mseko, Boza na Mivumoni.(watatu watazawadiwa).
Mashindano
haya yalianzishwa mwaka 2010 ili kuleta msukumo, ushindani na chachu ya
utekelezaji wa mipango ya vijiji ya ukimwi na maendeleo ya kijiji kwa
ujumla na kuotesha mbegu ya uwajibikaji.
Mwaka
2010 Kamati ya Sanga iliibuka mshindi, mwaka 2011 kamati ya Langoni,
iliibuka mshindi, mwaka 2012 kamati ya Langoni iliibuka mshindi tena.
Mwaka 2013 kamati ya Mseko iliibuka mshindi na mwaka 2014 Mseko iliibuka
mshindi tena.
Mwaka
huu wa 2015 mchuano ulikuwa mkubwa na kamati zimejituma na kuwajibika
katika utekelezaji wa mipango yao ya maendeleo pamoja na kuyasaidia
makundi mbalimbali yenye uhitaji.
Kamati
kumi 15 zimetekeleza vizuri. Kamati 12 zimetekeleza wastani. kamati 6
ikiwepo, Ushongo, Kipumbwi, Masaika, Kigurusimba, kimang,a na Mivumoni
zinahitaji msukumo wa ziada kwa Kukosa uwajibikaji.
Mashindano
haya yameleta msukumo katika shughuli zote za kiuongozi na maendeleo
ya vijiji. Palipo na uongozi mzuri na utekelezaji mzuri unakuwepo pia.
UZIKWASA
itaendelea kuwajengea uwezo viongozi wangazi zote na wanajamii kuweza
kujitathmini, kuzama na kujichunguza na kuweza kufanyia kazi changamoto
za kiuongoza na kuwezesha maendeleo katika jamii.
Suala la kupinga
unyanyasaji wa wanawake na watoto wa kike litapewa kipaumbele.
Kaimu mgeni rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bi.Patricia akizungumza na wananchi waliohudhuria katika tamasha hilo.
Burudani ya ngoma ilikua sehemu ya tamasha hilo.
Washehereshaji wa tamasha hilio, Pili Mlindwa na Shabani Kizamba wakiwajibika.
Mkurugenzi wa shirika la Uzikwasa na Meneja wa Pangani FM.
Wanakamati
wa kijiji cha Mseko katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa
washindi, na wameibuka washindi kwa mwaka wa 3 mfululizo.
Mmoja wa wanakamati ya VMACK ya kijiji cha mseko akicheza kwa furaha mbele ya meza kuu baada ya kutangazwa washindi.
Kaimu Mgeni rasmi Bi.Patricia akiwa ameshika ngao ambayo ni zawadi ya washindi wa VMACK kwa mwaka 2015.
Katibu wa kamati hiyo akipokea zawadi, Ngao na Hundi ya shilingi laki sita.
Vijana
bora wa mfano wa kuigwa walioingia katika hatua ya 3 bora, na
aliyeibuka mshindi ni kijana aliyevaa tshirt rangi ya njano.
Wamama
walioingia katika tatu bora mama mfano wa kuigwa, na aliyeibuka mshindi
ni mama ambaye ameshikilia pochi, ambaye anajulikana kwa jina maaarufu
kuti kavu.
Hapa akipokea zawadi ya hundi ya shilingi laki 1 kwa kua mama/mwanamke bora mfano wa kuigwa kwa mwaka 2015.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Jaira akigawa zawadi ya sare za shule kwa viongozi wa
vijiji vyote vya Wilaya ya PANGANI kwa niaba ya Aliyekua kijana bora
mfano wa kuigwa mwaka 2013-2014,ambayo aliahidi kwa watoto yatima
alipochaguliwa.
Wamama wakifurahia jambo.
Sehemu/baadhi
ya wananchi waliohudhuria katika tamasha la kuzizawadia kamati bora za
kudhibiti UKIMWI, kijana bora na mama bora wa mfano wa kuigwa kwa mwaka
2015 zilizofanyika katika kijiji cha JAIRA kata ya MADANGA Wilayani
PANGANI.
Waandishi
wa habari kutoka redio PANGANI FM, iliyochini ya shirika la UZIKWASA
wakifuatilia kwa makini tamasha hilo (waliovaa tshirt za PANGANI FM).
Wananchi wa Pangani waliofika katika kijiji cha Jaira wakifuatilia kwa ukaribu tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment