Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
Serikali
ya Tanzania imepoteza jumla ya Sh48.47bilioni baada ya makontena 11,884 na magari 2,019
kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi.
Hata hivyo,
jumla ya watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na Jeshi la Polisi
kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa mapato.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema ufisadi huo umebainika baada ya
serikali kuzifanyia ukaguzi bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini Dar es
Salaam.
Akifafanua,
Waziri Mbarawa amesema makontena hayo 11,884 yalikuwa na thamani ya Sh 47.4
bilioni wakati magari gari 2019 zenye thamani ya sh 1.07bilioni yalitolewa
bandarini pasipo kulipiwa tozo.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment