Baadhi ya
waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na
Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo,December 28,2015…Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Na Zainabu
Hamis wa Globu ya Jamii.
JUMLA ya
watu 493 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu Tanzania bara tokea
ulipoibuka jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na
Waandishi wa habari ofisini kwake leo, amesema kuwa jumla ya watu 12,222
wameugua ugonjwa huo tangu ugonjwa huo wa mlipuko kuaza hapa nchini.
“Ugonjwa wa
Kipindupindu umeanza tokea tarehe Desemba 15, 2015 katika mkoa wa Dar es salaam
na kusambaa katika mikoa 21 ya Tanzania” Mhe. Mwalimu amesema.
Hata
hivyo,Waziri huyo,amesema waathirika wa kipindupindu wameanza kupungua katika
mikoa ya Mwanza,
Arusha, Mbeya na Dar es salaam.
Pia ameitaja
Iringa na Kilimanjaro kuwa ni mikoa ambayo imeweza kuthibiti ugonjwa huo
hatari.
Waziri Mwalimu
akitoa takwimu za ugonjwa huo, amesema hivi sasa kuna wagonjwa wapya 76, hivyo
idadi ya wagonjwa wapya imefikia 493 na kifo kimoja.
“Hadi sasa
mkoa wa Morogoro vijijini unaongoza kwa wagonjwa 56, ukifuatiwa na Arusha (28),
Rorya (22), Bunda (21) na Kigoma vijijini 17.” Mhe. Mwalimu amesema”
Aidha
Mhe.Mwalimu ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuwa ni marufuku kuuza
matunda yaliyokatwa barabarani,kuuza vyakula katika mazingira yasiyo safi na
salama,huku akitaka kuandaliwa kwa taarifa za kila wiki kuhusu ugonjwa huo.
Akitoa rai
kwa wakuu wa wilaya na mikoa, kuwa walete taarifa sahihi za mlipuko wa ugonjwa
huo kwa ajili ya kuudhibiti. Na kwa kuwasisitiza watanzania kunywa maji safi na
salama na kunawa mikono kwa maji safi na salama.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment