Mmoja wa
watuhumiwa hao akiwa ndani ya gari la Polisi.
Katika
shtaka la pili, washtakiwa wanatuhumiwa katika ya Juni Mosi na Novemba 17 mwaka
huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam walishindwa kutimiza majukumu yao kwa namna
inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata hasara ya sh. bilioni 12.7.
Baada ya
washtakiwa hao kusomewa makosa yao, Hakimu Shahidi aliwaeleza kuwa mahakama
hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo hawatakiwi kujibu chochote
kama kweli au si kweli.
Aliongeza
kuwa Mahakama Kuu ndiyo inamamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo kama
wanataka dhamana wapeleke maombi ya dhamana katika mahakama hiyo.
“Kama
mnataka dhamana pelekeni maombi Mahakama Kuu kwa sababu mahakama hii hawezi
kutoa dhamana,” alisema Hakimu Shahidi
Hata hivyo,
upande wa utetezi ulidai kuwa kesi hiyo ifikishwa mahakamani hapo bila kibali
na pia waliomba mshtakiwa namba nne Mrema anamtoto mchanga kwa hiyo wanaiomba
mahakama imfikirie.
Wakili
Msigwa alidai upelelezi bado unaendelea, wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Kesi hiyo itatajwa Desemba 17 mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa
umekamilika.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii).
|
No comments:
Post a Comment