Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria
katika mkutano na Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), Dk. Philip Mpango jijini Dar es Salam leo.
Na
ChalilaKibuda,Globu ya Jamii
Baada ya
Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kufanya ziara ya kushitukiza katika Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) na kubaini upotevu wa Makontena 329, mapya yaibuka kwa
Makampuni 43 kuhusika kukwepa kodi ya Sh.Bilioni 12.6 katika Bandari Kavu
inayomilikiwa na Said Salim Bakh ressa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Desember 04,2015 Kaimu Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa
kampuni hizo 43 zilipitishiwa Kontena katika Bandari Kavu ya Said Salim
Bakhressa na kutaka ndani ya siku sita kuanzia leo kampuni zote ziwe
zimeshalipia kodi kutokana na idadi ya kontena.
Dk. Mpango amesema katika kampuni ambazo zilizokwepa kodi ambazo zilipitisha
Kontena 329 wameshalipa zaidi ya Sh. Bilioni Tano(5) ambapo wanatakiwa kulipa
kodi iliyobaki kuweza kumaliza kodi ya Sh.Bilioni 12.6 kwa kipindi alichoweka Rais
Dk .John Pombe Magufuli.
Amesema kuwa hatilafu za kupotea kwa makontena hayo, kazi hiyo walishakuwa
wameanza kwa bahati mbaya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Majaliwa aliwawahi
wakati alipofanya ziara katika mamlaka hiyo.
Kampuni zilizokwepa Kodi ya mapato kwa makontena 329 ni Lotai Steel Tanzania
LTD yenye makontena 100,Tuff Tyres Centre Company kontena 58 Binslum Tyres
Company LTD, Kontena 33, Tifo Global Mart (Tanzania) Company Limited Kontena
30,IPS Roofing Campany Ltd Kontena 20,Rashywheel Tyre Center Com.Ltd Kontena
12, Kiungani Trading Company Ltd 10 Homing International Limited Kontena 9, Red
East Building Kontena Saba,Tybat Trading Co Ltd, Kontena Tano,Zing Ent
Ltd,Kotena Nne,Juma Kassem Abdul, Kontena Tatu, Salum Continental Co.Kontena
Mbili, Zuleha Abbas Ali Kotena Mbili na Snow Leopard Building Kontena mbili na
waliobaki walikuwa na kontena moja moja.
Hata hivyo TRA imewasimamisha kazi watu 35 wakiwemo 27 waliokamatwa katika geti
namba tano ambao hadi sasa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano na uchunguzi.
Aidha amewataka wafanyakazi kuwasilisha mali zao ili kuweza kuangalia uwezo
wake katika utumishi kama zinaendana na umiliki huo.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment