PREMIER LEAGUE 2015/2016:-Man City, Tottenham na Liverpool zashinda Mechi zao za Nyumbani Leo December 26,2015, Chelsea sare - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 26, 2015

PREMIER LEAGUE 2015/2016:-Man City, Tottenham na Liverpool zashinda Mechi zao za Nyumbani Leo December 26,2015, Chelsea sare

Manchester United imeshushiwa kipigo chake cha 4 mfululuzo na Stoke City walioshinda 2-0 katika Mechi ya Ligi Kuu Uingereza 2015/2016 na Stoke walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 19 baada ya Pasi ya Geoff Camerok kwa Johnson kunaswa na Mchezaji wa Man United Memphis Depay lakini Kichwa chake hafifu cha kumrudishia Kipa wake De Gea kilitua kwa Johnson ambae haraka alimpasia Bojan Krkic na kufunga Bao laini.

Stoke City walipiga Bao lao la Pili Dakika ya 26 kupitia Marko Arnautovic baada ya Frikiki ya Bojan Krkic kuzuiwa na Ukuta wa Man United na kutua kwake na kuachia Shuti toka Mita 20.
Nyota wa Manchester United, Memphis Depay akiruka kichwa bila mafanikio kumuokoa kipa wake David de Gea, lakini akashindwa kumzuia Glen Johnson kuifungia Stoke City katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Mashetani hao Wekundu, bao lingine likifungwa na Marko Arnautovic Uwanja wa Britannia

Wakati Manchester City, Tottenham na Liverpool zikishinda Mechi zao za Nyumbani hii Leo December 26,2015, Chelsea, wakiwa kwao Stamford Bridge, walianza himaya ya Meneja mpya Guus Hiddink kwa Sare ya 2 – 2.

Chelsea walitangulia kufunga katika Dakika ya 32 kwa Bao la Diego Costa na Watford kusawazisha kwa Penati iliyotolewa baada ya Nemanja Matic kuushika Mpira na Penati hiyo kufungwa na Troy Deeney katika Dakika ya 42.

Watford walikwemba mbele 2-1 kwa Bao la Odion Ighalo la Dakika ya 56 na Diego Costa kufunga Bao lake la Pili Dakika ya 65 na kuipa Chelsea Sare ya 2-2.

Mwishoni Oscar alikosa Penati ambayo ingeweza kuwapa ushindi Chelsea katika Mechi ya kwanza ya Meneja wao mpya Guus Hiddink.

Huko Etihad, Man City ilicharuka na kuibonda Sunderland Bao 4-1 kwa Bao za Raheem Sterling, Yaya Toure, Wilfried Bony na Kevin De Bruyne huku Bao la Sunderland likifungwa na Fabio Borini.

Ushindi huu bado umewaweka City Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Arsenal na Pointi 3 nyuma ya Vinara Leicester City ambao Leo wamechapwa 1-0 na Liverpool huko Anfield kwa Bao la Christian Benteke.

Huko White Hart Lane, Tottenham waliichapa Norwich City Bao 3-0 kwa Bao za Harry Kane, Bao 2 na moja ni Penati, na la 3 kufungwa na Tom Carroll.

Jumamosi Desemba 26,2015.
 
Aston Villa 1 - 1 West Ham        

Bournemouth 0 - 0 Crystal Palace                  

Swansea 1 - 0 West Brom          

2030 Newcastle v Everton             

2245 Southampton v Arsenal

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad