TAARIFA YA
MAKABIDHIANO RASMI YA OFISI IKULU.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Novemba 12,2015,
katika Ikulu ya Dar es Salaam amepokea
taarifa rasmi ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete.
Makabidhiano
hayo yamefanyika mchana na kushuhudiwa
na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue na Maafisa wa Ofisi Binafsi ya Rais.
Utaratibu wa
kukabidhiana Ofisi katika Ofisi Kuu hapa nchini ni jambo la kawaida na hivyo imebidi makabidhiano hayo kati ya Rais anayeondoka na anaye ingia madarakani
kufanyika.
“Umeanza vizuri,
baki na msimamo huo huo utasaidia sana wananchi” . Mhe. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne amemueleza
Mhe. Rais Magufuli wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.
Mhe.Rais
Mstaafu amekabidhi taarifa rasmi yenye kurasa 53, ambayo kwa ujumla inaelezea
kazi zilizokwisha kufanyika, ambazo zinasubiri kukamilika na zile ambazo
zinasubiri maamuzi ya utekelezaji. Mengine ni
hali halisi ya nchi katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe.Rais
Dkt. Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi kwa muongozo wake siku zote
.“Nikushukuru kwa kuiacha nchi salama na itaendelea kuwa salama, nikushukuru
kwa muongozo wako, na taarifa ya
muelekeo na ninaahidi kuwa Hapa ni Kazi Tu”.
Mhe. Rais amesema na kumueleza Rais Mstaafu
kuwa ametengeneza mazingira mazuri ambayo nchi nyingi zimeshindwa kufanya na
hivyo basi kuahidi kuendelea kuchota hekima na busara kwa Marais wote wastaafu
wakiwemo Mhe. Benjamin William Mkapa wa
Awamu ya Tatu na Mzee Ally Hassan Mwinyi wa Awamu ya pili.
Wakati huo
huo Mhe. Rais Magufuli ameendelea kupokea salamu za pongezi kutoka Kwa
Msimamizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bibi Helen
Clark.
“Chini ya
uongozi wako, tunatarajia kuzidi kuimarisha ushirikiano baina yetu, demokrasia,
kushughulikia masuala ya umaskini na ajira kwa vijana , kukuza uchumi, na kulinda na kuhifadhi mazingira, masuala
ambayo Tanzania na UNDP tumekuwa tukishirikiana kuyaendeleza na kuyatimiza” amesema Bi Clark.
Salamu zingine
ni kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Uswiss, Mhe. Simonetta Sommaruga,Rais wa
Jamhuri ya Italia Mhe. Sergio Mattarella, Rais wa Jamhuri ya Shirikishola
Ujerumani Mhe. Joachim Gauck na pia kutoka kwa Rais wa Finland Mhe. Sauli Niinisto.
Pongezi zingine
zimetoka kwa Rais wa Jamhuri ya Urusi, Mhe. Vladimir Putin, Rais wa Jamhuri ya
Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Park
Geun-hye na kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. XI Jinping.
Salamu pia zimemfikia Mhe. Rais Dkt. Magufuli kutoka
kwa Rais wa Taifa la Eritrea Mhe. Isaias
Afwerki na kutoka kwa Rais wa Ufaransa Mhe. Francois Hollande.
Katika ujumbe
wao, viongozi hao mbali na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, wamesisitiza kuendeleza
na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zao.
Pia wameipongeza
Tanzania kwa kudumisha demokrasia imara na Watanzania kwa ujumla kwa kuimarisha
amani na utulivu wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa
Habari wa Rais, Msaidizi.
Ikulu,
DAR ES
SALAAM.
Novemba 12,
2015.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment