Aliyekuwa
daktari wa timu ya Chelsea, Eva Carneiro (42) mwenye shela pichani ) amefunga
ndoa na mshauri wa biashara aitwaye Jason De Carteret katika Kanisa la St.
Patrick jijini London November 11,2015.
Eva
anakumbukwa sana na mashabiki wa soka kwa kuwa daktari wa Chelsea tangu mwaka
2011 baada ya kupewa nafasi ya kuwa daktari wa kikosi cha kwanza na kocha wa
zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas.
Tangu hapo
amefanya kazi na makocha wengine kama Roberto di Matteo, Rafa Benitez hadi
alipokuja kusimamishwa kuingia uwanjani na Jose Mourinho mwezi Agosti mwaka huu,2015.
Eva aliingia
katika mgogoro na Jose Mourinho baada ya kuingia uwanjani haraka akiwa na
daktari mwingine, Jon Fearn kwenda kumtibu Eden Hazard wakati wa pambano kati
yao na Swansea na hivyo kuiacha Chelsea ikicheza pungufu ikiwa na wachezaji
tisa uwanjani huku ikisaka bao la ushindi.
Katika
mchezo huo, Mourinho anaamini kuwa Hazard hakuwa ameumia isipokuwa alikuwa
amechoka, hivyo kitendo cha madaktari hao kuingia uwanjani huku tayari kipa
Thibaut Courtois akiwa amepewa kadi nyekundu kiliipunguza kasi Chelsea kusaka
bao la ushindi.
Katika
harusi hiyo hakuna mchezaji yeyote wa Chelsea aliyehudhuria isipokuwa wachezaji
wa zamani wa timu hiyo akiwemo kipa Mark Schwarzer ambaye kwa sasa anachezea
klabu ya Leicester City.
Hapa chini tazama Picha za tukio hila la Harusi ya Eva
|
No comments:
Post a Comment