Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Yamungu
Kayandabila akizungumza na wadau wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
katika mkutano maalum wa siku ya Sayansi Duniani. Kushoto kwake ni Afisa
utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha ambaye alimwakilisha
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO- Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues. Mkutano huo
ulifanyika katika ukumbi wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam Novemba
10. 2015. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
Tanzania kupitia wadau wa Sayansi nchini
imedhamilia kupiga hatua zaidi katika kufikia malengo ya Agenda 2030 kwa
kuchangamkia fursa za maendeleo katika Sayansi.
Hayo
yameelezwa jijini hapa wakati wa wadau wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, walipokutana katika majadala wa Siku ya Sayansi Duniani kwa
ajili ya Amani na Maendeleo (World Science Day for Peace and
Development).
Akisoma
neno, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Dkt. Yamungu Kayandabila amelipongeza Shirika la Kimataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), katika kukuza Sayansi nchini.
Dkt.
Yamungu ameelezea kuwa, nchi yoyote ile ilikuendelea, inategemea
Sayansi hivyo kwa Tanzania ni wakati wa kuchangamkia fursa ili kufikia
malengo na Agenda 2030.
“Tanzania
tuna fursa nyingi na za kutosha. Tuna Nyuklia na hii ni uchumi tosha
tutakapofanyia kazi kwa malengo tutafika mbali kwani inahitaji Sayansi
ya kina.
Navipongeza
vyuo mbalimbali vilivyopo nchini ikiwemo DIT, Nelson Mandela cha
Arusha, Chuo cha Sayansi Mbeya na vingine vingi” ameeleza Dk. Yamungu.
Aidha,
Dkt. Yamungu ametaka Sayansi kuendana na suala la ulinzi wa chakula na
miundombinu mingine ikiwemo suala la maji huku akihimiza wanafunzi
kuyapenda na kuyasoma masomo ya Sayansi na suala la umuhimu wa Sayansi
na namna inavyoweza kuathiri maisha ya watu kila siku.
Afisa
Utawala na Fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha ambaye alimwakilisha Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa UNESCO- Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues
akisoma ujumbe maalum wa siku ya Sayansi Duniani wakati wa mkutano huo
wa wadau wa Sayansi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Prof. Evelyn Mbede
amepongeza wadau wa Sayansi na Teknolojia kwa kujimuika katika
maadhimisho ya siku hiyo ya Sayansi Duniani ambapo ameelezea kuwa Wizara
yake milango ipo wazi kwa wadau wote katika kuhakikisha wanapiga hatua
katika kukuza na kuendeleza Sayansi hapa nchini.
Kwa
upande wake, Afisa Utawala na Fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha ambaye
alimwakilisha Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO- Tanzania, Bi.
Zulmira Rodrigues alipongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika
kutilia mkazo suala la Sayansi na Teknolojia na kufanya suala hilo kuwa
mtambuka kwa maendeleo ya vizazi vya sasa na baadae.
Akisoma
ujumbe maalum kutoka UNESCO, Bw. Bokosha alieleza kuwa kupitia
Sayansi na Teknolojia na ubunifu, maendeleo ya Taifa endelevu,
uimarishaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa maandalizi
kwa ajili ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi na madhara yake
hivyo Sayansi inahitajika kwa kiwango kikubwa juu ya hilo.
Aidha,
ameeleza kuwa, UNESCO imekuwa mstari wa mbele katika kuanzishwa kwa
moduli za elimu ya Mazingira katika shule za Sekondari.
Profesa
John Kondoro Mkuu wa Chuo cha Teknolojia cha jijini Dar es Salaam –
(DIT) akitoa mada katika mkutano huo wa wadau wa Sayansi wakati wa
maadhimisho ya siku ya Sayansi.
Akinukuu ujumbe maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova katika ujumbe alieleza:-“Hii
ni siku ya Sayansi Duniani kwa amani na Maendeleo na imekuja miezi
miwili baada ya makubaliano ya Agenda 2030 ya maendeleo endelevu.
Hivyo
Serikali zote zitambue nguvu ya Sayansi ya kutoa majibu muhimu kwa
usimamizi mzuri wa maji kwa ajili ya hifadhi na matumizi endelevu ya
bahari, ulinzi wa mazingira na viumbe hai, ilikukabiliana na mabadiliko
ya tabianchi na majanga na kuendeleza uvumbuzi na kuondokana na
umasikini na kupunguza tofauti” alieleza katika nukuu hiyo.
Afisa kutoka UNESCO NAT.COM, Bw. Joel Samuel akitoa mada katika mkutano huo wa wadau siku ya Sayansi Duniani.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, akifafanua jambo wakati wa mjadala
huo juu ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia nchini katika mkutano
uliowakutanisha wadau wa Sayansi katika maadhimisho ya Siku ya Sayansi
Duniani.
Wadau
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa siku ya Sayansi Duniani.
No comments:
Post a Comment