SHERIA YETU:-Mwanajeshi feki akamatwa Mkoani Kigoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, November 03, 2015

SHERIA YETU:-Mwanajeshi feki akamatwa Mkoani Kigoma.

Mwanajeshi feki ( PICHANI) wa Jeshi la wananchi (JWTZ) amekamatwa November 02,2015, Mkoani Kigoma akiwa amevaa sare za Jeshi hilo na kuwatapeli fedha baadhi ya watu.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya tukio hilo ,Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Fednandi Mtui alisema kuwa mwanajeshi huyo feki alikamatwa  eneo la kazuramimba katika Wilaya ya uvinza.

Kamanda Mtui alisema kuwa mwanajeshi huyo alitambulika kwa jina la James Charles miaka 27 mkazi wa kijiji cha Nyamori, alikamatwa baada ya kuwepo kwa taarifa kutoka kwa raia wema juu ya utapeli aliokuwa akiwafanyia na kuwekewa mtego na kukamatwa.

Kamanda alisema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa na kuulizwa alipozitoa sare hizo alisema kuwa yeye ni dobi wa kufua nguo,hivyo huvaa sare hizo pale anapoletewa na wateja kwa ajili ya kuzifua.

Amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akijifanya Ofisa wa JWTZ na Ofisa wa uhamiaji na amekamatwa akiwa tayari amewatapeli wananchi shilingi Milioni Moja ambapo alikuwa ameshachukua shilingi Laki moja kati ya hizo
  
Alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika,pia jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi wote ambao wameshatapeliwa na mtuhumiwa huyo kutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi kilichopo jirani yao.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad