KUAPISHWA RAIS TANZANIA:-Dkt. MAGUFULI anaapishwa, kesho November 05,2015 ni mapumziko. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 04, 2015

KUAPISHWA RAIS TANZANIA:-Dkt. MAGUFULI anaapishwa, kesho November 05,2015 ni mapumziko.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

November 5, 2015,Ni siku ambayo Watanzania watashuhudia kuapishwa kwa Rais wa awamu ya tano atakayeongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano inayofatia.


Tayari kutoka Ikulu , ambapo Rais anayemaliza muda wake, Dkt.Jakaya Kikwete ametangaza siku ya kesho November 05 2015 kuwa siku ya mapumziko ili kuwapa fursa Watanzania kushuhudia tukio hilo.

Hii ni sehemu ya taarifa iliyosambazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu,Balozi Ombeni Sefue.

Ikulu new
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.

Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Novemba, 2015.



Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad