RAHA YA USHINDI:-Tazama Bw Alex Gashaza akikabidhiwa Hati ya Ushindi ya Ubunge Jimbo la Ngara Mkoani Kagera - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, November 03, 2015

RAHA YA USHINDI:-Tazama Bw Alex Gashaza akikabidhiwa Hati ya Ushindi ya Ubunge Jimbo la Ngara Mkoani Kagera

Picha ya pamoja ya Mbunge Mteule wa jimbo Ngara, Bw Alex Gashaza (CCM) Mwenye shati la kijani akiwa na baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali kwenye ukumbu wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara,mkoani Kagera  jana November 02,2015 wakati Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Ngara Bw Kelvin Makonda akimkabidhi Hati ya ushindi.

Kutoka kushoto ni Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Ngara na Mkurugenzi Mtendaji wilaya,Bw Kelvin Makonda  akiteta jambo na Mkuu wa wilaya hiyo Bi Honoratha Chitanda.

Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika , Bi Honoratha Chitanda amemtaka Bw Gashaza kushirikiana na wakazi wa Jimbo hilo kutatua kero zinazowakabili bila kujali itikadi zao kisiasa.

Bi Honoratha amesema yuko tayari kushirikiana na Bw Gashaza katika uongozi wake ili kuharakisha maendeleo ya wilaya ya Ngara.

Baada ya kukabidhiwa Hati hiyo, Bw Gashaza amewashukuru wakazi wa Ngara kwa kumpa dhamana hiyo kuahidi kuwa mwaminifu na muadilifu katika kuwatumikia

Pia amewaomba kuendelea kumuombea wakati huu anapoelekea Dar es Salaam kisha Dodoma Bungeni kwa ajili ya kuapishwa na kwamba atakaporejea atafanya ziara jimboni mwake.. 


Mkoa wa Kagera una  jumla ya majimbo ya uchaguzi 9 ambayo ni:-

Bukoba Mjini: Wilfred Lwakatare (CHADEMA)

Bukoba Vijijini: Rweikiza Jasson (CCM)

Biharamulo: Oscar Rwegasira Mukasa (CCM)

Karagwe: Innocent Luugha Bashungwa (CCM)

Kyerwa: Innocent Sebba Balikwate (CCM)

Muleba Kusini: Prof. Anna Tibaijuka(CCM)

Nkenge - Deodorius Kamala (CCM)

Ngara: Bw. Alex Gashaza (CCM)
 

Habari na Radio Kwizera FM.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad