![]() |
Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na wanahabari (hawapo
pichani).
|
Picha ya juu na chini ni Waandishi wa
habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
|
Nape akijiandaa kujibu maswali ya wanahabari yaliyokuwa yameulizwa
(hawapo pichani).
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kipo kwenye mchakato wa kumtafuta
mgombea wake wa Ubunge Jimbo la Handeni mkoani Tanga baada ya kutofanyika
uchaguzi kufuatia kifo cha mgombea wake kwa tiketi ya chama hicho, Abadallah
Kigoda.
Akizungumza na wanahabari November 02,2015, kwenye ofisi za chama hicho zilizopo mtaa
wa Lumumba jiijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
amesema kuwa, wajumbe wa kamati ya CCM wapo kwenye mchakato huo na kesho
mgombea atapatikana.
Alisema kamati hiyo imeshachuja waliojitokeza kuomba nafasi hiyo ambao
walikuwa 11 na sasa wamebaki wawili ambao ni Hamis Hamad na Omar Kigoda hivyo
kesho watakaa kikao cha kumpata mgombea mmoja.
NA DENIS MTIMA/GPL
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment