NDEGE KUANGUKA SINAI, MISRI:-Hii ndio Taswira Picha ya Mabaki yake Tazama Hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, November 03, 2015

NDEGE KUANGUKA SINAI, MISRI:-Hii ndio Taswira Picha ya Mabaki yake Tazama Hapa.

Muonekano wa Mabaki ya Ndege ya Shirika la Kogalymavia la Urusi, Airbus A-321 iliyoanguka eneo la Sinai nchini Misri ilikuwa na abiria 200, watoto 17 na wafanyakazi wa ndege hiyo 7 ,ambapo Watu wote 224 waliokuwa katika ndege hiyo waliaga dunia.

Miili ya watu 160 waliofariki dunia katika ajali ya ndege eneo la Sinai nchini Misri iliwasili mjini St Petersburg nchini Urusi.




Wachunguzi wakiwa eneo la tukio wakiangalia mabaki ya Ndege ya Shirika la Kogalymavia la Urusi, Airbus A-321 iliyoanguka eneo la Sinai nchini Misri ilikuwa na abiria 200, watoto 17 na wafanyakazi wa ndege hiyo 7.


Mabaki ya Ndege aina ya Airbus A-321 iliyoanguka siku ya Jumamosi ikitokea Mji wa Sharm el-Sheikh ikielekea mji wa St. Petersburg nchini Urusi.


Mmoja wa wachunguzi wa masuala ya safari za ndege kutoka Urusi amesema kuwa ndege ya Urusi iliyoanguka katika rasi ya Sinai nchini Misri ilivunjika ikiwa hewani.

Aleksandr Neradko amesema kwamba mabaki ya ndege hiyo yametapakaa katika rasi ya Sinai.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad