MO katika
picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Makampuni ya MeTL Group, Vipul Kakad mara
baada ya kutwaa tuzo hiyo.
Mo ametwaa
tuzo hiyo kwa kuwashinda watu watano mashuhuri barani Afrika. Watu hao ni
Nkosazana Dlamini Zuma, mke wa Kwanza wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
Mama huyo kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU). Mwingine ni Rais
wa sasa wa Nigeria, Muhammadu Buhari aliyetambuliwa kutokana na kuanzisha vita
dhidi ya rushwa nchini mwake.
Aidha wapo
Arumna Otei, mchumi mahiri raia wa Nigeria ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa
Benki ya Dunia. Pia alikuwemo Mwandishi maarufu wa vitabu wa Nigeria, Chimanda
Ngozi Adichie ambaye moja ya vitabu vyake vinaelezea picha halisi ya Afrika
inavyofikiriwa duniani.
Akitoa neno
la shukurani baada ya kukabidhiwa kwa tuzo hiyo Mo, alisema anatoa tuzo hiyo
kwa vijana wa Kitanzania kwani ndio nguvu kazi inayobeba uchumi wa nchi.
Mo ambaye
kampuni yake ya MeTL inaongoza kwa kutoa ajira nchini, ikiwa imetoa ajira
26,000 kote katika viwanda vyake 31 vilivyopo nchini na katika mataifa matano
ya Afrika, alisema amefurahishwa na tuzo hiyo ambayo anaitoa kwa vijana kwa
kutambua pia wajibu mkubwa walionao katika kukabiliana na umaskini. BOFYA HAPA KUSOMA NA KUTAZAMA PICHA ZAIDI.
|
Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na Shemane Amin wakipitia moja ya taarifa iliyowavutia kwenye jarida la Forbes Afrika. |
MO katika
picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Jaguar Land Rover ambao
ni miongoni mwa wadhamini wa sherehe za tuzo hizo.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment