Mkuu wa Chuo cha VETA Makete, Ramadhan Sebo akitoa
nasaa kwa wanafunzi wanaoingia mtaani kujiajiri.
Watanzania wametakiwa kuwapelewa watoto wao
katika vyuo mbalimbali vya ufundi stadi elimu inayo zalisha ajira nyingi kuliko
vyuo vikuu hapa nchini ili kuepukana
na tatizo la ajira.
Inadaiwa kuwa watu wanaojiajiri ni wengi wanao toka katika vyuo vya ufundi kuliko
wanano maliza vyuo vikuu kutokana na wanao toka vyuo vikuu wanategenea kuajiliwa
huku wa vyuo vya ufundi wakijikita kujitengenezea ajira na kuachana na
utegemezi kutoka kwa wazazi.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa bodi ya vyuo
vya Veta nyanda za juu inayo
jumuisha mikoa ya Iringa, Ruvuma na Njombe, Kabaka Ndenda,juzi November 27,2015 katika mahafari ya
kwanza kwenye chuo pekee cha wilaya cha Veta Makete,alisema kuwa vijana
wengi wanao maliza katika vyuo vya ufundi
wanauhakika wa kujiajiri kuliko wanao enda vyuo vikuu.
Alisema kuwa wananchi wamekuwa wakiona
ni bora kumpeleka mtoto wake katika chuo
kikuu kuliko kumpeleka katika vyuo vya ufundi, alisema kuwa Tanzania kutokana na
ulivyo mfumo wa ajira watoto ni bora wakapelekwa katika vyuo vya ufundi ili
kutengeneza ajira.
“Tanzania tulikataa mfumo wa mwalimu
Nyerere wa ujamaa tukataka ukabaila wakati
hatuwezi kwenda nao ndio maana tunapata shida kupata ajira, Tanzania bado
hatujafika hatua ya kusoma vyuo vikuu na kupata ajira moja kwa moja,” alisems Ndenda.
Alisema kuwa licha ya vijana hao wanao
fuzu mafunzo kuweza kujiajiri wanatakiwa
kuhakikisha kuwa wakitoka hapo wanaenda kuunda vikundi ili waweze kukopesheka.
Hata hivyo wanafunzi hao waliiomba
serikali kuhakikisha kuwa inawapa sapoti pale
watakapo kuwa wameunda vikundi vyao na kuweza kujikwamua kimaisha kwa kupata mikopo
kutoka serikalini.
Mkuu wa chuo hicho Ramadhani Sebo
alisema kuwa wanafunzi hao wanaenda kuajirika licha ya
kuwa na changamoto za vifaa vya kufundishia katika baadhi ya fani zinazo
fundishwa katika vyuo hivyo ikiwa ni pamoja na katika fani ya ufundi magari.
Alisema kuwa wanafunzi katika chuo hicho
wamefanya mafunzo kwa vitendo na wameiva
vyakutosha kwenda kuingia katika kujiajiri katika ufundi na kuanza kujitegemea.
Alisema kuwa chuo hicho kwa sasa ambacho
ni chapekee cha wilaya Tanzania nzima na
kuwa kilianza na kozi mbili na sasa kina kozi 4 huku kikifundisha masomo
mtamboka.
Alisema kuwa kutokana na kuto kuwa na
mabweni chuo hicho wanafunzi wake wamepanga
mitaani na kuwa baadhi ya wanafunzi wameshindwa
kumaliza chuo kutokan ana
changamoto za kutoka mbali na kukutana na vishawishi. |
No comments:
Post a Comment