LIGI YA MABINGWA ULAYA 2015/2016:-FC Bayern Munich, Barcelona na Chelsea zashinda na matokeo ya mechi nyingine za November 4. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, November 05, 2015

LIGI YA MABINGWA ULAYA 2015/2016:-FC Bayern Munich, Barcelona na Chelsea zashinda na matokeo ya mechi nyingine za November 4.

Timu za FC Barcelona, Chelsea na Bayern Munich zilishinda katika mechi zao za klabu Bingwa barani Ulaya.

Kwa Matokeo ya Jana November 04,2015, FC Barcelona, Bayern Munich na FC Porto nazo zinakaribia kufuzu.

Wakati Barcelona ikichapa BATE Borisov kwa magoli 3 - 0 , Bayern Munich wao walitoa dozi ya magoli 5 - 1 kwa Arsenal.
Katika Mechi ya Marudiano ya Kundi G la UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2015/2016, hapo Jana November 04,2015 huko Stamford Bridge Jijini London, Meneja Jose Mourinho aliesakamwa yeye na Timu yake kwa matokeo mabovu Msimu huu, alipata ahueni baada ya kuifunga Dynamo Kiev Bao 2-1.

Matokeo kamili ya mechi zilizochezwa haya hapa chini,Sambamba na Msimamo wa makundi ulivyo.

Barcelona 3 - 0 BATE Bor

Bayern Munich 5 - 1 Arsenal

Chelsea 2 - 1 Dynamo Kiev

Roma 3 - 2 Bayer Levkn

Olympiakos 2 - 1 Dinamo Zagreb

M'bi Tel-Aviv 1 - 3 FC Porto

KAA Gent 1 - 0 Valencia

Lyon 0 - 2 Zenit St P
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad