BREAKING NEWS:-Dk. Magufuli aapishwa kuwa Rais wa Tano wa Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, November 05, 2015

BREAKING NEWS:-Dk. Magufuli aapishwa kuwa Rais wa Tano wa Tanzania.


Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ameapishwa leo,November 5, 2015, na wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Tanzania wanasema atakuwa na mzigo mzito wa kushughulikia ahadi na mambo kadhaa mazito yanayoachwa na mtangulizi wake, Rais Jakaya Kikwete.

Dk.Magufuli alishinda kwa zaidi ya asilimia 58 katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25,2015 na leo November 05,2015 ameapishwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, katika siku maalum iliyotangazwa kuwa ya mapumziko kitaifa ili kutoa fursa kwa kila Mtanzania kushuhudia.


Mamilioni ya Watanzania watatarajiwa nia ya kuanza kushuhudia ‘mabadiliko ya kweli’ aliyoahidi Magufuli wakati wa kampeni, bado kuna mambo mazito anayoachiwa na Rais Kikwete, na ambayo baadhi ya wafuatiliaji wa siasa za Tanzania wanayaelezea kuwa ni ‘mizigo’ mizito kwake.

Baadhi ya mambo hayo yanatajwa kuwa ni mgogoro ulioibuliwa upya wa hali ya kisiasa visiwani Zanzibar; katiba mpya na pia utekelezaji wa baadhi ya maazimio ya bunge kuhusiana na kashfa ya ulaji wa mabilioni ya fedha za akaunti ya Tegeta Escrow.


Kadhalika,  wafuatiliaji wa siasa za Tanzania wanataja mzigo mwingine mzito unaoachwa na Rais Kikwete kwa Rais mpya, Dk. Magufuli, ni utekelezaji wa ahadi kadhaa kubwa zilizowahi kutolewa tangu wakati wa kampeni na Rais Kikwete anayemaliza muda wake leo,November 05,2015.Bofya hapa kusoma zaidi Mizigo ya JK kwa Magufuli hii hapa.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad