KOMBE LA SHIRIKISHO AZAM SPORTS :-Ratiba yake yatoka ….Sasa rasmi kuanza November 08,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 04, 2015

KOMBE LA SHIRIKISHO AZAM SPORTS :-Ratiba yake yatoka ….Sasa rasmi kuanza November 08,2015.


Pichani ni kikosi cha Timu ya Rhino Rangers wataanza na Alliance Novemba 24, mwaka huu,2015.

 Michuano ya Kombe la Shirikisho ya AZAM SPORTS inafunguliwa rasmi Jumapili (Novemba 8, 2015) kwa mechi tatu zitakazochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti.

Mechi rasmi ya ufunguzi itakuwa kati ya wenyeji JKT Rwamkoma ya Mara na Villa Squad ya Dar es Salaam itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Siku hiyo pia kutakuwa na mechi kati ya Kariakoo ya Lindi na Changanyikeni FC ya Dar es Salaam itakayochezwa kwenye Uwanja wa Ilulu mjini Lindi, wakati Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Wenda FC ya Mbeya na Madini SC ya Arusha.

Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Azam Sports HD ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).

RATIBA YA AWALI


08.11.2015
1
JKT RWANKOMA
  VILLA SQUAD
KARUME-MUSOMA
08.11.2015
2
WENDA FC
  MADINI FC
SOKOINE
08.11.2015
3
KARIAKOO
  CHANGANYIKENI
ILULU
10.11.2015
4
SABASABA FC
  ABAJALO TABORA
MABATINI
10.11.2015
5
MILAMBO FC
  THE MIGHTY ELEPHANT
ALI HASSAN MWINYI
11.11.2015
6
SINGIDA UNITED
  BULYAKHULU SC
NAMFUA
11.11.2015
7
ABAJALO DAR
  TRANSIT CAMP
KARUME
11.11.2015
8
MKAMBA RANGERS
  MVUVUMWA
KILOMBERO
21.11.2015
9
AFC
  POLISI MARA
SHEIKH AMRI ABEID
21.11.2015
10
PAMBA SC
  POLISI DODOMA
CCM KIRUMBA
22.11.2015
11
PANONE FC
  COCACOLA KWANZA
USHIRIKA
22.11.2015
12
MAGEREZA IRINGA
  POLISI DAR
WAMBI MUFINDI
23.11.2015
13
POLISI TABORA
  GREEN WARRIORS
ALI HASSAN MWINYI
24.11.2015
14
RHINO RANGERS
  ALLIANCE
ALI HASSAN MWINYI
25.11.2015
15
RUVU SHOOTING
  COSMOPOLITAN
MABATINI
26.11.2015
16
POLISI MOROGORO
  MSHIKAMANO
JAMUHURI MOROGORO



Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad