LIGI KUU TANZANIA BARA 2015/2016:- Azam FC hao kileleni leo November 01,2015 wakimfunga Toto Africans 5 - 0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 01, 2015

LIGI KUU TANZANIA BARA 2015/2016:- Azam FC hao kileleni leo November 01,2015 wakimfunga Toto Africans 5 - 0.

Didier Kavumbangu (kushoto) amefunga mabao mawili leo Azam FC ikishinda 5-0

Klabu ya  Azam FC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2015/2016 baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Toto Africans kwenye mchezo wake Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni ya leo November 01,2015.

Ushindi huo unaifanya timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake ifikishe (Azam FC) pointi 25 baada ya kucheza mechi tisa, ikiwazidi kwa pointi mbili, mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 23.

Shomary Kapombe ndie aliefungua Mabao kwa kupachika Goli katika Dakika za 34 na 36 na kisha Kipre Herman Tchetche kuipa Azam FC Bao la 3 kwenye Dakika ya 45.

Kipindi cha Pili, Azam FC walifunga Bao la 4 baada ya Toto Africans kujifunga wenyewe na Didier Kavumbangu kupiga Bao la 5.

MATOKEO MECHI ZA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA 2015/2016.

Leo; Novemba 01, 2015

Prisons 2 - 2 Ndanda FC

African Sports 0 - 2 JKT Ruvu

Azam FC 5 - 0 Toto Africans

Jana; Oktoba 31, 2015

Simba SC 6 -1 Majimaji FC

Kagera Sugar 0 -2 Yanga SC

Mtibwa Sugar 4-1 Mwadui FC

Coastal Union 1-1 Mbeya City

Kesho; Novemba 02, 2015

Mgambo Shooting Vs Stand United


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad