Rais wa
Kenya, Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na kuwapiga
chini mawaziri wote ambao wizara zao zinakumbwa na kashfa za ufisadi.
Uamuzi wa
Rais Kenyatta umekuja siku moja baada ya kutangaza ufisadi kama tishio la
usalama wa kitaifa huku akiazimia kufanya mabadiliko makubwa kwenye ofisi ya
Rais hivi karibuni.
Katika
mabadiliko hayo, Kenyatta ameongeza pia idadi ya wizara kutoka 16 hadi 20 na
kuongeza idara mpya chini ya wizara hiyo, kutoka idara 26 hadi 41 kwa kile
alichoeleza kuwa ni kusaidia wizara kutekeleza majukumu yao bora zaidi.
Baadhi ya
mawaziri walikuwa tayari wamekwisha jiondoa kwenye wizara zao kwa tuhuma za
ufisadi huku wengine wakiwa na kesi za kujibu mahakamani.
Hivi
karibuni, Waziri wa Ugatuzi, Anne Waiguru alikuwa wa mwisho kujiondoa kwenye
wizara akiwa na kashfa zilizopata umaarufu zaidi kwa kipindi cha hivi karibuni
za kununua kalamu moja kwa shilingi zaidi ya 200,000 za Tanzania.
Hata hivyo,
Uhuru Kenyatta hakuwa na budi ya kuvunja baraza lake na kuunda upya kwa kuwa
katiba ya nchi hiyo inataka idadi ya mawaziri isiwe chini ya 14. Baada ya
Waiguru kujiuzulu nafasi ya uwaziri, baraza la mawaziri lilibaki na mawaziri 13
pekee.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment