Kocha wa
Taifa Stars Charles Mkwasa ameomba kucheza mchezo huo ili kupata nafasi ya
kuangalia kikosi chake kabla ya mchezo na Algeria.
Taifa Stars
wapo Johannesuburg Afrika Kusini kwa kambi ya siku 10 kabla ya kurejea Dar Es
Salaam kucheza mechi dhidi ya Algeria, Stars inafanya mazoezi asubuhi na jioni
kwa ajili ya kujiweka sawa na inatumia viwanja vya St. Peters College na kituo
cha michezo cha Edenvale.
|
Kuhusu hali
ya kambi, kocha mkuu wa Stars Charles Mkwasa amesema anashukru maendeleo ni
mazuri vijana wake wote wapo katika hali nzuri hakuna majeruhi na wanaendelea
na maaandalizi ya mchezo dhidi ya Algeria utakaopigwa Novemba 14 jijini Dar es
salaam.
Wachezaji 26
waliopo kambini ni magolikipa Ally Mustafa, Aishi Manula na Said Mohamed,
walinzi ni Shomari Kapombe, Juma Abdul, Ramadhan Kessy, Mohamed Hussein, Mwinyi
Haji, Hassan Isihaka, Salim Mbonde, Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub
“Cannavaro”.
Wengine ni
Himid Mao, Frank Domayo, Mudahir Yayha, Salum Abubakar, Said Ndemla, Jonas
Mkude, Salum Telela, Farid Musa, Saimon Msuva, Malimi Busungu, Elias Maguri,
John Bocco na Mrisho Ngasa.
Aidha
wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya
Congo DR, wanatarajiwa kuungana na kikosi cha Stars baada ya mchezo wao wa
fainali Ligi ya Mabingwa Afrika Jumapili dhidi ya USM Alger.
|
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. |
No comments:
Post a Comment