KLABU BINGWA ULAYA 2015/2016:-FC Barcelona na Bayern sasa zaungana na Real Madrid, Manchester City na Zenit Saint Petersburg kwenda mtoano wa timu 16. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 25, 2015

KLABU BINGWA ULAYA 2015/2016:-FC Barcelona na Bayern sasa zaungana na Real Madrid, Manchester City na Zenit Saint Petersburg kwenda mtoano wa timu 16.

Lionel Messi akimlamba chenga kipa wa Roma kuifungia bao la pili FC Barcelona wakati wa Mshikemshike wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2015/2016 hatua ya makundi usiku wa November 24,2015 katika viwanja mbalimbali barani Ulaya, kwa jumla ya mechi nane zinazohusisha timu kutoka Kundi E, F, G na H, na Mabingwa watetezi, FC Barcelona wameendelea kung’ara baada ya kuitandika AS Roma mabao 6-1 Uwanja wa Camp Nou na kufikisha pointi 13 Kundi E.
2EC783E400000578-0-image-a-20_1448397862932
Goli la pili la FC Barcelona lilifungwa na Lionel Messi dakika ya 18 ya mchezo kabla ya Luis Suarez kufunga goli la tatu dakika ya 44, goli la nne lilifungwa na Gerrard Pique dakika ya 56, Lionel Messi dakika ya 60 kabla ya Adriano kupachika goli la sita dakika ya 77, AS Roma ambao walikuwa hawaamini kilichowakuta walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi kutoka kwa Edin Dzeko dakika ya 90.

Mchezo mwingine wa kundi hilo, BATE Borisov imelazimishwa sare ya 1-1 na Bayer 04 Leverkusen bao lake likifungwa na Mikhail Gordeychuk dakika ya pili, kabla ya Admir Mehmedi kuwasawazishia wageni dakika ya 68 Uwanja wa Borisov Arena.

Roma na Bayer Leverkusen sasa zitaingia kwenye mechi za mwisho kuwania kuungana na Barcelona kwenda 16 Bora, sasa zote kila moja ikiwa na pointi 5.

Ushindi wa magoli 3-0 walioupata Arsenal wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Dinamo Zagreb umefufua matumaini ya klabu hiyo kusonga mbele kwenye michuano ya Ulaya baada ya Bayern Munich kuichapa timu ya Olympiakos ambao ndio wanawania nafasi na Arsenal ya kusonga kwenye hatua ya mtoano.

Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Mesut Ozil dakika ya 29 na Alexis Sanchez mawili dakika ya 33 na 69.

Matokeo hayo yanaifanya yanaifanya Arsenal ipate matumaini ya kusonga mbele lakini ikiwa na kazi nzito ya kutakiwa kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Olympiakos. 

Kwa sasa Arsena ipo nafasi ya tatu kwenye kundi F ikiwa na pointi 6, Bayern Munich ndiyo kinara wa kundi hilo ikiwa na jumla ya pointi 12 ikifuatiwa na Olympiakos yenye pointi 9.

Mechi nyingine ya kundi hilo usiku wa jana November 24, 2015, Bayern Munich wameitandika Olympiakos 4-0 mabao ya Douglas Costa de Souza dakika ya nane,
Robert Lewandowski dakika ya 16, Thomas Muller dakika ya 20 na Kingsley Coman dakika ya 70 Uwanja wa Allianz Arena.
Nayo Chelsea imeweka hai matumaini ya kutinga 16 Bora baada ya ushindi mnono wa ugenini wa mabao 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv katika mchezo wa Kundi G, ikipata mabao kupitia kwa Gary Cahill, Willian Borges Da Silva, Oscar dos Santos Emboaba Junior na Kurt Zouma .

Chelsea sasa inaongoza Kundi G kwa pointi zake 10, sawa na FC Porto pia – lakini bado watahitaji pointi tatu katika mchezo wa mwisho kujihakikishia kuipiku Maccabi  yenye pointi nane.

Mchezo mwingine wa kundi hilo, Dyanmo Kyiv jana November 24,2015,imeshinda ugenini nchini Ureno mabao 2-0 dhidi ya FC Porto, mabao ya Andriy Yarmolenko kwa penalti dakika ya 35 na Derlis Gonzalez dakika ya 64 Uwanja wa Estadio do Dragao.

Jumatano Novemba 25,2015.

KUNDI A

Malmö FF v Paris St Germaine   
          
Shakhtar Donetsk v Real Madrid 
         
KUNDI B

2000 CSKA v VfL Wolfsburg  
     
Man United v PSV Eindhoven  
            
KUNDI C

1800 FC Astana v Benfica   
       
Atletico Madrid v Galatasaray   
           
KUNDI D

Borussia Mönchengladbach v Sevilla  
             
Juventus v Man City     
 
 Matokeo ya mechi nyingine za Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizochezwa November 24,2015.

KUNDI E
  • BATE Borisov 1 – 1 Bayer Leverkusen
  • FC Barcelona 6 – 1 Roma
KUNDI F
  • Arsenal 3 – 0 Dinamo Zagreb
  • Bayern Munich 4 – 0 Olympiakos
KUNDI G
  • FC Porto 0 – 2 Dynamo Kyiv
  • Maccabi Tel Aviv 0 – 4 Chelsea
KUNDI H
  • Zenit St. Petersburg 2 – 0 Valencia
  • Lyon 1 – 2 Gent

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad