Rais John
Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipomtembelea
ofisini kwake Dar es Salaam jana November 26,2015. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu). |
Rais wa
Serikali ya awamu ya Tano ya Tanzania,Dr. John Magufuli ambaye tangu Novemba
17, mwaka huu 2015,alikuwa katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa majukumu
mbalimbali, amerejea Dar es Salaam jana,November 26,2015 na wakati wowote
inaelezwa kwamba anaweza kutangaza Baraza la Mawaziri linalosubiriwa kwa hamu
na Watanzania.
Dk Magufuli
alitua Ikulu ya Chamwino, Novemba 17 kwa kutumia usafiri wa barabara akisafiri
kwa zaidi ya kilometa 300 kwenda katika Makao Makuu ya Serikali ambako kwanza
alikuwa na majukumu mawili makubwa.
Novemba 19,
mwaka huu, alimteua Mbunge wa Ruangwa mkoani Lindi, Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu na siku iliyofuata
alimwapisha katika Ikulu hiyo iliyoko takribani kilometa 40 kutoka Dodoma
Mjini.
Aidha, baada
ya kumwapisha Majaliwa asubuhi, jioni hiyo ya Novemba 20, Dk Magufuli aliyeingia
madarakani Novemba 5, mwaka huu 2015, alilihutubia na kulizindua Bunge la 11
mjini Dodoma katika hotuba iliyosisimua wabunge na Watanzania kwa ujumla kwa
kugusa kero na mipango mbalimbali anayokusudia kuifanya.
Dk Magufuli
alirejea Dar es Salaam huku tetesi zikiimarika kwamba atatangaza baraza lake la
mawaziri siku yoyote kuanzia jana November 26,2015, na aliondoka Dodoma kwa
ndege majira ya saa mbili asubuhi.
Kuwapo kwake
kwa siku nyingi katika kijiji cha Chamwino akifanya kazi, kulipongezwa na
wanakijiji hao. Aidha, wanazuoni na wanasiasa walitafsiri uwapo wake kijijini
hapo kuwa ni kujichimbia asibughudhiwe wakati akipanga baraza lake la mawaziri
na mfumo wa uendeshaji mpya wa baraza hilo.
Na ishara au
dalili kwamba Baraza la Mawaziri limeiva au litatangazwa wakati wowote ni hatua
ya Dk Magufuli kutua Dar es Salaam na baadaye mchana kwenda ofisini kwa
Majaliwa ambako ni jirani na Ikulu ya Magogoni.
Kwa mujibu
wa Katiba ya Tanzania, Rais atateua Baraza la Mawaziri kwa kushauriana na
Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, hivyo kuna kila dalili wawili hao kama sio wote
watatu, wameshafanya kazi hiyo. SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA
|
No comments:
Post a Comment