Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha afya Kambarage
mjini Shinyanga ili kujionea hali halisi jinsi huduma zinavyotolewa kwa
wananchi siku moja tu baada ya muuguzi wa kituo hicho kukamatwa kwa
tuhuma ya kuiba dawa za serikali.
Pichani ni mkuu wa wilaya Josephine
Matiro na katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga wakiwa katika chumba cha
kuhifadhia dawa wakiwa wamepigwa butwaa baada ya kuona chumba
kimesheheni dawa wakati mara kwa mara wananchi wamekuwa wakiambiwa
hakuna dawa badala yake wanaambiwa wakanunue kwenye maduka ya watu
binafsi mtaani-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Hapa ni ndani ya ofisi ya mganga
mkuu/msimamizi wa kituo hicho ambapo mkuu wa wilaya akiwa ameambatana na
maafisa wengine wa manispaa ya Shinyanga amekutana na uongozi wa kituo
hicho pamoja na wananchi waliomkamata muuguzi mkunga wa kituo hicho
Joseph Nkila akituhumiwa kuiba dawa za serikali.Kulia ni Rashid Shaban
akimweleza mkuu huyo wa wilaya jinsi walivyofanikisha kufichua wizi huo
Wa pili kutoka kulia ni msimamizi wa
kituo cha afya Kambarage Dkt Nassoro Yahya akitoa maelezo kwa mkuu wa
wilaya ya Shinyanga kuhusu suala la upungufu wa dawa katika kituo chake
ambapo alisema kituo kina upungufu wa dawa na walishatoa taarifa
panapohusika siku nyingi zilizopita.
Hata hivyo maelezo yake yalipingana
na yale ya kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dkt Mhana
Raphael(mwenye suti pichani) aliyedai kuwa mkoa wa Shinyanga hauna
tatizo la upungufu wa dawa bali dawa pekee ambayo haipo ni ile ya
Antibiotic
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro akizungumza katika kituo cha afya cha Kambarage mjini Shinyanga
ambapo pamoja na mambo mengine amemwagiza mkurugenzi wa manispaa ya
Shinyanga kumsimamisha kazi muuguzi Joseph Nkila anayetuhumiwa kuiba
dawa za serikali pamoja na msimamizi wa kituo hicho Dkt Nassoro Yahya
kwa uzembe unaosababisha mwanya wa upotevu wa dawa katika kituo hicho na
kusababisha wananchi kuilalamikia serikali kwa kukosa dawa wakati mkoa
wa Shinyanga hauna tatizo la dawa
Mfamasia/mtunza dawa wa kituo cha afya
Kambarage Seleman Hamza akitoa maelezo namna anavyofanya kazi katika
kituo hicho ambayo hata hivyo mkuu wa wilaya hakuridhika nayo na
kumwagiza yeye na msimamizi wa kituo waandae maelezo ya kina ndani ya
siku 5
Mmoja wa wasamaria wema waliomkamata
muuguzi anayedaiwa kuiba dawa akisimulia jinsi wizi wa dawa
unavyofanyika katika kituo hicho na jinsi walivyomkamata Joseph Nkila.Soma hapa Maelezo yake na wenzake
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akiwa
katika kituo cha afya Kambarage,nyuma yake ni katibu tawala wa wilaya ya
Shinyanga Boniface Chambi na kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga
Sande Deogratius
Dawa zikiwa katika chumba cha kuhifadhia dawa cha Kituo
Mfamasia/mtunza dawa wa kituo cha afya
Kambarage Seleman Hamza akizungumzia kuhusu tukio la wizi wa dawa
katika kituo hicho na changamoto ya dawa katika kituo hicho ambapo
alisisitiza kuwa kuna baadhi ya dawa hazipo katika kituo hicho
Dawa zikiwa katika chumba cha kuhifadhia dawa kituo cha afya Kambarage
Dawa katika kituo cha afya Kambarage
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro na
katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi wakiwa katika
chumba cha kuhifadhia dawa
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoka kwenye kituo cha afya Kambarage
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro akitoa maelekezo kwa kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga
Dkt Mhana Raphael(mwenye suti),kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga
Sande Deogratius na mfamasia wa manispaa ya Shinyanga Emmanuel Zabron
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akimpa
maelekezo kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dkt Mhana-Picha
zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Hapa Kazi tu ndiyo Tunaweza Kusema!! Novemba 26,2015 asubuhi..Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro anafanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha afya cha Kambarage katika manispaa ya Shinyanga ili kujionea hali halisi ya huduma zinazoendelea katika kituo hicho.
Hapa Kazi tu ndiyo Tunaweza Kusema!! Novemba 26,2015 asubuhi..Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro anafanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha afya cha Kambarage katika manispaa ya Shinyanga ili kujionea hali halisi ya huduma zinazoendelea katika kituo hicho.
Kubwa zaidi lililomfikisha hapo asubuhi asubuhi ni kuhusu sakata la muuguzi wa kituo hicho Joseph Nkina kukamatwa na wananchi akiwa na dawa za serikali ikiwemo kopo moja la dawa aina ya paracetamol na chupa mbili za dawa ya maji aina ya Erythromycin kinyume na utaratibu.
Baada ya kukutana na uongozi wa kituo hicho na wananchi waliofanikisha kukamatwa kwa muuguzi mkunga wa kituo hicho Joseph Nkila amemwagiza mkurugenzi wa manispaa hiyo kumsimamisha kazi muuguzi huyo kuanzia jana Novemba 26,2015, ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo.
“Nimekuja hapa kuona uhalisia wa jambo hili,Kuna ushihidi wa wazi kabisa kuwa muuguzi huyu kweli kaiba dawa za serikali,mbaya zaidi akataka kudanganya kwa kuchukua stakabadhi kutoka kwenye duka la dawa za binadamu (pharmacy), nimekutana na msimamizi wa kituo cha afya Kambarage na mfamasia anayetunza dawa,na kinachoonekana hapa ni uzembe kwenye uongozi kwani dawa zinatoka bila kufuatiliwa kuwa dawa hizo zinafanya nini”,amefafanua Matiro.
“Nitamshangaa sana hakimu atayepindisha kesi hii kwani ushahidi uko wazi kabisa kutoka kwa wananchi kwamba amekuwa akijihusisha na wizi kwa muda mrefu na kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu katika kituo hiki cha afya,wananchi wananyimwa dawa,kumbe watu wachache tu wanacheza mchezo huu mchafu wa kuiba dawa”,-ameeleza Matiro.
“Kila siku wananchi wanalalamika hakuna dawa,lakini tumeangalia stoo tumekuta dawa zipo za kutosha na Shinyanga hatuna tatizo la dawa,dawa moja tu ambayo ni Antibiotic ndiyo haipo,na tumeagiza iletwe”,-alieleza Matiro.
“Cha kusikitisha msimamizi wa kituo
hiki Dkt Nassoro Yahya anasema hakuna upotevu wa dawa,huyu naye hatakiwi
kuwa hapa kazi imemshinda,nimemwagiza mkurugenzi pia amsimamishe kazi
kwani haiwezekani dawa zitoke kwenye kituo bila yeye kufahamu”,-amesema
Matiro.
Katika hatua nyingine Matiro amewashukuru na kuwapongeza wananchi waliofanikisha kumkamata muuguzi huyo na kuahidi kuwapa zawadi kwa kazi nzuri waliyofanya akiwataka wananchi wengine kuendelea kuwafichua watumishi wasiofanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi zao Mkuu huyo wa wilaya ametoa onyo kwa muuguzi aliyekamatwa,ndugu na marafiki kuacha kutoa vitisho kwa wananchi waliokamata dawa hizo na kufanikisha juhudi za kukamatwa kwa muuguzi huyo kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukulia dhidi yao.
No comments:
Post a Comment