THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua
wakuu wa wilaya wapya 13 na kuwahamisha vituo vya kazi wengine saba.
Wakuu
wa wilaya 13 walioteuliwa ni Shaaban Athuman Ntanambe ambaye anakuwa Mkuu wa
Wilaya ya Chato, Mkoa wa Kagera; Thabisa Mwalapwa ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya
ya Hanang, Mkoa wa Manyara; Richard
Kasesera ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa, Ruth Msafiri
ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma na Abdallah Njwayo
ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Wakuu
wa Wilaya wengine wapya ni Asumpta Mshama ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya
Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe; Mohammed Mussa Utaly ambaye anakuwa Mkuu wa
Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma; Dauda Yasin ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya
Makete, Mkoa wa Njombe; Honorata Chitanda ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya
Ngara, Mkoa wa Kagera; Vita Kawawa ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama,
Mkoa wa Shinyanga na Christopher Ng’ubyagai ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama,
Mkoa wa Singida.
Wakuu
wengine wapya ni Hawa Ng’humbi ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mkoa
wa Shinyanga na Mrisho Gambo ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mkoa wa
Kigoma.
Wakuu
wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ni Fadhili Nkurlu ambaye anatoka
Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda Wilaya ya Arusha, Mkoa wa Arusha; Wilson E
Nkambaku ambaye anahamishiwa Arumeru, Mkoa wa Arusha kutoka Kishapu, Mkoa wa
Shinyanga; Francis Miti ambaye anahama Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara kwenda
Monduli, Mkoa wa Arusha na Jowika Kasunga ambaye anahamia Wilaya ya Mufindi,
Mkoa wa Iringa kutoka Monduli .
Wengine
waliohamishwa ni Muhingo Rweyemamu kutoka Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe kwenda
Wilaya ya Morogoro; Hadija Nyembo ambaye anahamia Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa
Tabora kutoka Uvinza, Mkoa wa Kigoma na Benson Mpyesya ambaye anahamia Wilaya
ya Songea, Mkoa wa Ruvuma kutoka Kahama.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
04 Oktoba, 2015
Na hapo jana tarehe
3.10.2015, Mh. Rais amefanya uteuzi mwingine akama taarifa hii kwa vyombo vya
habari inavyoonyesha:
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais
waJ amhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Ndugu Francis M. Mwakapalila kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali kuanzia juzi,
Alhamisi, Oktoba 1 , 2015.
Ndugu
Mwakapalila anachukua nafasi ya Bibi Mwanaidi Mtanda ambaye amestaafu kazi kwa
mujibu wa sheria.
Kabla
ya uteuzi wake kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, Ndugu Mwakapalila alikuwa Naibu
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
03 Oktoba, 2015
WAKATI HUO HUO, LEO,
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete ametuma slamu zake za rambi rambi :
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma
salamu za rambirambi na maombolezo kumlilia Mwenyekiti wa Chama cha Siasa cha
Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ambaye alipoteza maisha
katika ajali ya gari iliyotokea alfajiri ya leo, Jumapili, Oktoba 4, 2015,
katika Kijiji cha Msolwa, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Katika
salamu zake za rambirambi kwa Chama cha DP, Rais Kikwete amesema: “
Nimepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wenu na Mtanzania
mwenzetu, Mchungaji Christoher Mtikila ambaye nimeambiwa amepoteza maisha
katika ajali ya gari Mkoani Pwani akiwa njiani kurejea mjini Dar es Salaam
akitokea kwao Njombe.”
“Kwa
hakika, kifo cha Mchungaji Mtikila ni pigo kubwa kwa Chama cha Democratic Party
ambacho kimempoteza kiongozi wake mkuu. Aidha, kifo hicho ni pigo kwa medani za
siasa katika Tanzania na kimetunyang’anya mmoja wa viongozi hodari na wazalendo, aliyekuwa na msimamo thabiti na
usioyumba katika kutetea mambo ambayo aliyaamini katika maisha yake yote,”
amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Ni
jambo la kusikitisha pia kuwa tunampoteza Mchungaji Mtikila katika kipindi cha
mchakato muhimu wa kisiasa nchini ambako mchango wake ulikuwa unahitajika sana.
Hakika, tutamkosa mwenzetu katika uwanja wa siasa za nchi yetu.”
Ameendelea
Rais Kikwete, “Nawatumieni nyie wana-democratic Party salamu za dhati ya moyo wangu
na pole nyingi kwa kuondokewa na kiongozi wetu mkuu, wa miaka mingi na wenye uzoefu
wa uongozi wa chama cha siasa.”
“Aidha
kupitia kwenu, napenda kuitumia pole zangu nyingi familia ya Mchungaji Mtikila.
Nawapa pole sana wanafamilia, ndugu na marafiki na napenda wajue kuwa niko nao
katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mhimili wa familia. Naungana
nao katika majonzi. Aidha, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi
wa Rehema, aiweke pema roho ya Mchungaji Christopher Mtikila. Amen”.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
04 Oktoba, 2015
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Monday, October 05, 2015
Home
HABARI
UTEUZI WA RAIS 2015:- Wafahamu Wakuu wa Wilaya wapya 13 na kuhamisha Wakuu wa wilaya saba na Vituo vyao vya Kazi.
UTEUZI WA RAIS 2015:- Wafahamu Wakuu wa Wilaya wapya 13 na kuhamisha Wakuu wa wilaya saba na Vituo vyao vya Kazi.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment