October
05 2015 ni siku ya pili inaisha tangu litokee tukio la ajali ya gari ndogo
jana October 04,2015 ,katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze Mkoa wa Pwani ambapo ndani yake kulikuwa na
watu watatu pamoja na Mwanasiasa Mkongwe Tanzania, Mchungaji Christopher Mtikila ambaye alifariki kutokana
na ajali hiyo.
Tangu
kutokea kwa ajali hiyo mambo mengi yameongelewa kuhusu ajali na kifo chake,
mazingira ya ajali? Marehemu kutokuwa na jeraha? Mchungaji kufariki na wengine
kupona? Ripoti ya Hospitali? Mazishi?
Familia
ya Mchungaji Mtikila imeweka kila kitu
sawa >>>> “Mchungaji Christopher Mtikila alipata ajali majira ya saa 11 Alfajiri eneo la Msolwa
Chalinze, bahati mbaya alikuwa hajafunga mkanda na gari ilikuwa speed… Kulikuwa
na gari llilikuwa lime-overtake upande wao, dereva wao akakwepa kwenda kushoto“.– Victor
James Manyai, Msemaji wa Familia.
Habari kwa hisani ya MILLARDAYO.COM
|
Victor James Manyai, Msemaji wa Familia.
Hapa
Msemaji wa Familia anasimulia mazingira ya ajali ilivyokuwa >>> “Eneo lile barabara imeinuliwa juu zaidi na eneo la pembeni
limeshuka chini.. gari lilipaa juu, liliposhuka chini matairi yakapasuka yote,
kwa sababu hakuwa amevaa mkanda akatokea mbele ya kioo cha gari.. alipoenda
kuangukia, gari likaenda kumfunika upande wa kushoto, akawa hawezi kupumua“.- Victor
Manyai.
|
Watu
wengine walitoka na Majeraha kwenye gari, nini kilifanya Mchungaji
afariki pekeyake? >>> “Ilichukua muda kwa
sababu walikuwa watu wanne, mmoja alikuwa ameumia zaidi, mwingine alitupwa
mbali… ilibidi mpaka wasamalia wema waje kusaidia kumuinua… walijaribu
kumsaidia lakini hakuweza kupumua tena“.
|
Baadhi ya waombolezaji wakiwa
msibani.
Kuna
stori kwenye Mitandao ya Kijamii kuhusu kifo chake huku wengine wakihoji
kwa nini mwili wa Mchungaji Mtikila haujaonekana
kuwa na majeraha yoyote? >>> “Mimi
nilikuwepo katika Kikosi cha watu waliofanya postmortem pale Kibaha, tulikuwa
na madaktari wanne, madaktari wawili wa Familia, mmoja wa Polisi na mmoja wa
Hospitali ya Kibaha… sio kweli kwamba hana majeraha, alikuwa na majeraha
kichwani na miguuni, ila siwezi kutaja siri za Marehemu ni kinyume cha
maadili... Ukweli ni kwamba alikosa hewa, na kama kungekuwa na msaada wa
dharura maisha yake yangeokolewa…“>>>
|
Mke wa Marehemu Mchungaji Mtikila.
Gari
alilopata nalo ajali je? >>> “Ukweli ni
kwamba gari lilikuwa limekodiwa, Mchungaji alikuwa na magari mawili na yote
yalikuwa katika Kampeni Mkoa wa Mara na jingine Wilaya ya Kahama… Mimi ndio
nilimkodia gari kwa madereva wa Taxi Mbezi mwisho, ni vijana ambao nawafahamu.”
>>>
|
Hii
ndio Taarifa ya Familia kuhusu taratibu za kuaga Mwili wa marehemu na
Mazishi >>> “Mwili wa Marehemu kwa sasa
upo Hospitali ya Lugalo, Jumatano tutaaga mwili wa Marehemu Karimjee au Leaders
Club, baada ya hapo tutasafirisha mwili kwenda Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe”
>>> Victor James Manyai, Msemaji wa Familia ya Marehemu Mchungaji
Mtikila.
|
RIP Mchungaji Christopher Reuben Mtikila.
Sauti ya Msemaji wa Familia imesikia kwenye
Amplifaya October 05 2015, # kama ulipitwa unaweza kuisikiliza pia hapa.
|
No comments:
Post a Comment