UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015:-Dr. Magufuli Akabidhiwa Rasmi CHETI Cha Ushindi wa Kiti cha Urais wa Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, October 30, 2015

UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015:-Dr. Magufuli Akabidhiwa Rasmi CHETI Cha Ushindi wa Kiti cha Urais wa Tanzania.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania bara -NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amemkabidhi cheti cha ushindi wa kiti cha URAIS, Dk John Pombe Magufuli  na  mgombea  mwenza  wake, Bi.  Samia  Suluhu  katika  Ukumbi wa Diamond Jubilee  asubuhi  ya leo hii October 30,2015.

 Katika  tukio  hilo, Wagombea urais wa Chadema Edward Lowassa na Hashim Rungwe wa Chauma wamesusia sherehe hizi  za kukabidhiwa cheti cha ushindi Dk John Magufuli wa CCM.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema kuwa Magufuli, alijipatia kura 8,882,935 ikiwa ni aslimia 58.46.

Mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa wa chama cha Chadema alijipatia kura 6,072,848 ikiwa ni asilimia 39.97 ya kura zote halali.

Baada ya kutangazwa kwa ushindi wake, wafuasi wake walisherehekea katika miji mbalimbali nchini humo.
Msafara wa Rais mteule John Magufuli pamoja na ule wa Rais Jakaya Kikwete waelekea ikulu chini ya ulinzi mkali.
Mgombea urais wa chama cha ACT Wazalendo Anna Mghwira aliyemaliza wa tatu ni miongoni mwa waliofika kumpongeza Bw Magufuli.

Rais anayeondoka Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria hafla hiyo, sawa na kiongozi wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Madola Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan. Bw Jonathan amampongeza rais mteule.
John Pombe Joseph Magufuli akabidhiwa rasmi cheti cha ushindi uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili Oktoba 25,2015.

Hafla ya kumkabidhi Magufuli cheti inafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad