TASWIRA PICHA :-Dk. Magufuli na Mama Samia kuanzia ukumbini mpaka Ofisi za CCM. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, October 30, 2015

TASWIRA PICHA :-Dk. Magufuli na Mama Samia kuanzia ukumbini mpaka Ofisi za CCM.

Jina la aliyekuwa Waziri Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli lilianza kubeba headlines za uzito zaidi kipindi ambacho na yeye alitangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea Urais kwa kuchukua Fomu kutoka Makao Makuu ya Chama Dodoma, baadae akateuliwa… akapita kwenye Kampeni na hatimaye matokeo ya Uchaguzi wa October 25 2015 yakampitisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

.
Kwenye picha ya pamoja, hapo ni Dk. Magufuli, Mama Samia Suluhu, Jaji Damian Lubuva na baadhi ya Wagombea waliokuwa wakigombea kiti cha Urais Tanzania kwenye Uchaguzi wa mwaka 2015.

Tume ya Uchaguzi NEC imekamilisha kazi yake ambapo leo October 30 2015 Dk. Magufuli na mgombea mwenza wake ambaye atakuwa Makamu wa Rais Serikali ya awamu ya tano, Mama Samia Suluhu Hassan wamekabidhiwa rasmi vyeti vya kuthibitisha ushindi wao kwenye nafasi hizo.

Kazi ya vyeti ilikuwa pale Ukumbi wa Diamond Jubilee, eneo la Upanga Dar es Salaam na baada ya hapo msafara ukaelekea katika Ofisi za CCM zilizopo mtaa wa Lumumba , Dar es Salaam.
.
Naibu Spika aliyemaliza muda wake, Job Ndugai.

.
Kamanda wa Polisi Ernest Mangu akisalimiana na Jenerali Davis Mwamunyange.

.
Hapa ni IGP Ernest Mangu, Jen. Mwamunyange akisalimiana na DC wa Kinondoni, Paul Makonda.
.
.
.
Baadhi ya waalikwa walioshuhudia tukio hilo Ukumbi wa Diamond Jubilee, ikiwemo viongozi wa dini pamoja na wengine ikiwemo Mzee Reginald Mengi.

.
Mzee Reginald Mengi na Jenerali Davis Mwamunyange.

.
Mzee John Malecela, Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba akimwangalia jeraha la mkononi Nape Nnauye.

.
Dk. Magufuli akikabidhiwa Cheti na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva.. yuko pia Mama Samia Suluhu na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima.

.
Picha ya kumbukumbu: Rais Kikwete, Mama Salma, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Dk. Magufuli, Mama Samia, Jaji Damian Lubuva, pamoja na Mama Janeth Magufuli.

.
.
.
.
.
.
Screen Shot 2015-10-30 at 1.58.05 PM
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad