![]() |
Didier Kavumbangu (kushoto) akishangilia na Farid Mussa baada ya kufunga bao la kwanza leo October 29,2015. |
Klabu ya Azam FC imefanikiwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2015/2016 baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 4-2 jioni ya leo October 2015,kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kufikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi nane, ikiwazidi pointi mbili mabingwa watetezi, Yanga SC ambao jana October 28,2015,walilazimishwa sare ya 2-2 na Mwadui mjini Shinyanga.
Kwa ushindi wa leo, sifa zimuendee mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu ambaye amefunga bao moja na kuseti mengine mawili, moja la John Bocco na lingine la Kipre Tchetche.
![]() |
Didier Kavumbangu akipiga shuti kufunga bao la pili pembeni ya beki wa JKT Ruvu, Michael Aidan |
![]() |
MATOKEO YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
Oktoba 29, 2015.
Prisons 1-0
African Sports
JKT Ruvu 2-4 Azam FC
Oktoba 28, 2015.
Toto African 1-0 Mgambo Shooting
Mwadui FC 2-2 Yanga SC
Mtibwa Sugar 1-0 Kagera Sugar
Mbeya City 1-1 Majimaji FC
Ndanda FC 0-0 Stand United
Simba Sc 1-0
Coastal Union
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment