Chopa
iliyosababsha kifo cha Filikunjombe, Capt. William Silaa na watu wengine
wawili jana Jioni, October 15,2015.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Mapinduzi Bw Deo Filikunjombe
amefariki kutokana na ajali ya Helikopta iliyotokea kwenye hifadhi ya wanyama
ya Selous, pamoja na rubani Kepteni William Silaa, mfanyakazi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Ludewa, wakati
akitokea Dar es Salaam kwenda Ludewa.
Wengine
waliofariki kwenye ajali hiyo ni Vitalis Blanka Haule na Ofisa Tawala wa Wilaya
ya Tarime, Bw. Egdi Mkwera ambaye alikuwa mtaalam wa mifugo.
Kamishna wa
oparesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini Bw Paul Chagonja amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo ikihusisha Helikopta yenye namba 5Y - DKK katika kijiji cha
Mtende mkoani .
Kamishna
Chagonja amesema polisi na taasisi nyingine ikiwemo mamlaka ya usalama wa anga
wameanza uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya helikopta inayodaiwa kuwa
ilikuwa imekodiwa na Bw Deo Filikunjombe. |
No comments:
Post a Comment