TANZIA:-Taswira Picha walivyoagwa Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta October 15, 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 18, 2015

TANZIA:-Taswira Picha walivyoagwa Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta October 15, 2015.

Miili ya marehemu watatu kati ya wanne waliokufa kwenye ajali ya chopa (helikopta) iliyotokea usiku wa kuamkia jana, Oktoba 16, 2015 katika Hifadhi ya Selous, eneo la Msolwa mkoani Morogoro, imeagwa leo jinini Dar es Salaam.

Shughuli ya kuaga miili ya marehemu hao ilianzia katika hospitali ya Lugalo ambapo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete aliwaongoza mamia ya Watanzania kuaga miili ya marehemu hao ambao ni aliyekuwa Mbunge wa jimbo la ludewa, Mhe. Deo Filikunjombe (43), Plasdius Ngabuma Haule na Egdi Francis Mkwera aliyetajwa kuwa Ofisa Tawala wa Wilaya ya Tarime.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo Waziri Mkuu anayemaliza muda wake, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge Anne Makinda, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe Magufuli, ndugu, jamaa na marafiki.

Baada ya kumaliza kuaga hapo Lugalo, miili ya marehemu ilipelekwa nyumbani kwa Deo Filikunjombe maeneo ya Mtoni Kijichi jijini Dar, kwa ajili ya kuagwa ndugu na majirani. 

Zoezi hilo lilitanguliwa na ibada fupi ya kuombea miili ya marehemu hao kabla ya kuagwa na kusafirishwa kwa ndege kwenda nyumbani kwao Ludewa Njombe kwa mazishi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli  akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta , Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimfariji Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe.
 
Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe akilia kwa uchungu kufuatia kifo cha Mumwe Deo Filikunjombe,wakati wa kuaga katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 
Dkt Magufuli akifarijiana na Mh.Zitto Kabwe  wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. 
 
Dkt Magufuli alishindwa kujizuia kutoa machozi ya huzuni  wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
  Majeneza yenye miili ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe na ndugu zake, Plasdus Ngabuma na Casablanga Haule yakiwa yamewekwa mbele ya waombolezaji  wakati wa kuaga katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. kabla ya kusafirishwa kwenda Ludewa kwa mazishi mkoani Njombe.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.  

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad