Wananchi wa
Mji wa Monduli wakionyesha upendo wao kwa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa, pindi
alipowasili katika Uwanja wa Polisi Monduli, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni
zake, Oktoba 5, 2015.
|
Mgombea wa
nafasi ya urais kwa kitiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda
umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa ,akiwa mjini Monduli
amewaahidi kuhakikisha anakuwa mstari wa mbele katika kutetea na kuimarisha
maendeleo ya wana monduli na watanzania kwa ujumla.
Awali
akihutubia mikutano ya hadhara wilayani Monduli katika maeneo ya Ingaruka,
Loksari, Makuyuni na Monduli mjini amesema bado ni dhamira yake kuona
watanzania wananufaika na rasilimali amabzo zimewazunguka.
Mgombea huyo
wa nafasi ya urais na timu yake ya kampeni ameendelea kupata uungwaji mkono na
idadi kubwa ya wananchi ambapo leo Jumanne October 06,2015 anatarajia kuanza
ziara ya kampeni zake mjini Same mkoani Kilimanjaro.
|
Mgombea
Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA,
Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli kwa tiketi ya
CHADEMA, Julius Kalanga, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja
wa Polisi, Monduli Mjini Oktoba 5, 2015.
|
Waziri Mkuu
wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia Wananchi wa Mji wa Monduli, wakati
wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye
Uwanja wa Polisi, Monduli Mjini leo Oktoba 5, 2015.
|
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli
kwa tiketi ya CHADEMA, Julius Kalanga, akizungumza machache juu namna
atakavyoweza kuendeleza pale alipoaishia Mbunge wao wa awali.
|
Mh. Joshua Nassary
wa Arumeru Mashariki akitema cheche zake.
|
Mgombea
Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA,
Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa Zamani, Fredrick Sumaye, wakionyesha lundo la
kadi za wanachama wa CCM wa Wilaya ya Monduli, waliozirudisha ili kuungana na
Watanzania wote kwenye harakati ya Mabadiliko, wakati wa Mkutano wa Kampeni
uliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi, Monduli Mjini Oktoba 5, 2015. ...Kulia ni
Aliekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Monduli, Rubein Ole Kuney akiejiunga na
Chadema.
|
Aliekuwa
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh. Joshua Nassary, akizikusanya kadi za
Wanachama wa CCM zilizorudishwa na kujiunga na Chadema, wakati wa Mkutano wa
Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi, Monduli Mjini jana Oktoba 5, 2015.
|
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI........
|
No comments:
Post a Comment