Magufulika Style inavyozidi kushika kasi,Davis Mosha mgombea
ubunge jimbo la Moshi mjini na madiwani wa Moshi mjini wakimagufulika jukwaani
kuonyesha ukakamavu wao.
|
Sehemu ya Umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika
viwanja vya mashujaa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe
Magufuli,jana October 07,2015, jioni kwenye mkutano wa kampeni,mkoani Kilimanjaro.
Katika mkutano wake wa Moshi mjini Dkt. Magufuli amewaonya watendaji wa
Shirika la Umeme nchini TANESCO na kuwaambia kama wanazima umeme makusudi ili
kuwafanya wananchi waichukie serikali wanafanya makosa na ole wao kwa vitendo
hivyo visivyo vya kistaarabu, Amewaambia kwamba bado siku 17 za kampeni
akichaguliwa na wananchi na kuapishwa kuwa Rais atawashughulikia ipasavyo
kwani wanajulikana. “Katika siku hizi zilizobaki watubu
wafanye kazi usiku na mchana ili umeme upatikane bila kukatika na kuleta adha
kwa wananchi vinginevyo akiingia Ikulu atalala nao mbele”,alisema Dkt Magufuli
huku uwaja mzima ukilipukwa kwa mayowe.
|
Sehemu ya Umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika viwanja
vya mashujaa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,leo
jioni kwenye mkutano wa kampeni,mkoani Kilimanjaro.
|
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia
umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika viwanja vya mashujaa
Kumsikiliza alipokuwa akijinadi na kuwaga sera zake katika kuomba kura za
kuwania nafasi ya Urais kwa kipindi cha awamu ya tano,kwenye uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
|
Sehemu ya Umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika
viwanja vya mashujaa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe
Magufuli,jana October 07,2015, jioni kwenye mkutano wa kampeni,mkoani Kilimanjaro alipokuwa
akijinadi na kuomba kura za kutosha ili aibuke kuwa Rais wa Tanzania wa awamu
ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment