KAMPENI UBUNGE 2015 /NGARA:-CHADEMA yaahidi kuboresha miundombinu ya elimu sambamba na kuwalipa walimu posho ya kufundishia. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, October 01, 2015

KAMPENI UBUNGE 2015 /NGARA:-CHADEMA yaahidi kuboresha miundombinu ya elimu sambamba na kuwalipa walimu posho ya kufundishia.

Ni taswira ya Madawati Pichani yalipokutwa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ngara mkoani kagera kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Dr Petter Bujari, Katika shule ya Rwinyana,wilayani Ngara mkoani Kagera kwenye mkutano wake wa kampeni September 29,2015 ambapo alikuta Wanafunzi wa madarasa matatu wanakaa nje na ‘’Nimeahidi kuwa CDM/CHADEMA itaboresha miundombinu ya elimu sambamba na kuwalipa walimu posho  ya kufundishia’’...

Nimekuta madarasa ya watoto ( Madawati yako chini ya mti) nikaambiwa madarasa matatu yako nje chini ya mti. 

Wananchi walipaza zauti hata chaki wanananunua wenyewe.

Sehemu ya umati wa watu waliofika kwenye mkutano wa Dk Bujari, Uwanja wa Kijiji cha Rwinyana,wilayani Ngara mkoani Kagera.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ngara mkoani kagera kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Dk Petter Bujari alifanya Kampeni zake katika Kijiji cha Rwinyana  ambapo alishuhudia  na kuambiwa na Wananchi  changamoto mbalimbali zinazowakabili,’’- Katika zahanati ya Mumilamila, nimekuta mhudumu mmoja tu. Analalamika kuwa hana Likizo na hapaswi kuugua. Wananchi wanalalamika anawatoza faini wakijifungukia njiani au nyumbani. Kadi za kliniki wanauza sh. 3000 wakati haziuzwi. 

Nimezisitiza kuwa wananchi wahamasishwe kujifungulia hospitali siyo kutozwa faini.

 Pia kuwa CDM/CHADEMA tutaongeza watumishi wa afya.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.    

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad