Mwanahabari
na blogger wa mtandao wa modewjiblog.com, Andrew Chale akiwa katika geti
kuu la kuingilia katika ofisi za Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa zilizopo
eneo la Mang'ula, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro, Tanzania.
Alipokuwa
katika habari za Utafiti jinsi ya Mabadiliko ya Tabianchi yanavyoathiri
mbuga na hifadhi za Taifa nchini (How Climate Change Effect The National
Parks in Tanznia) hivi karibuni (Picha na modewjiblog).
TABIANCHI YAWEKA HIFADHI ZA TANZANIA HATARINI
Na Andrew Chale, modewjiblog
Zimebaki siku zaidi ya 60, kuelekea mkutano mkuu wa 21 (COP21) wa nchi
wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Nchi (UNFCCC) unaotarajiwa kufanyika
Paris, Ufaransa. mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.
Dulu
na chunguzi za kitafiti zinaeleza kuwa, Tanzania ni miongoni
mwa Mataifa Barani Afrika yatakayokumbwa na janga kubwa dhidi ya
Mabadiliko ya tabianchi (Climate Change in Tanzania National Parks)
kwenye Hifadhi na mbuga zake.
Dulu
hizo za kitafiti pia zinabainisha kuwa, asilimia kadhaa za Wanyama nao
watatoweka kabisa hali ambayo taifa litakumbwa na matatizo mbalimbali ikiwemo
kushuka kwa uchumi wa Nchi katika siku za usoni.
Hivi
karibuni, mwandishi wa Makala haya wa modewjiblog, alipata kutembelea Hifadhi
kadhaa za taifa zilizo chini ya usimamizi wa Shirika la Hifadhi la Taifa,
Tanzania National Parks Authority (TANAPA).
Hifadhi
hizo zikiwepo Udzungwa, Selous Game Reserve, Mikumi, Ruha,
na Saadan pamoja na kuonana na wataalamu wa mabadiliko ya tabianchi
kwenye idara za serikali na watu binafsi.
Eneo la kuingia katika Hifadhi na makao makuu ya hifadhi ya Udzungwa...
Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa:
Kwa mujibu wa tovuti ya Serikali inabainisha kuwa Udzungwa ni
miongoni mwa milima yenye Bionuwai nyingi iliyozungukwa na misitu.
Hata hivyo vyanzo mbalimbali vinabainisha kuwa, Hifadhi hii ya
Udzungwa ni miongoni mwa Hifaadhi zilizo kwenye hatari ya kutoweka kutokana na
mipango hafifu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Vyanzo vya ndani vinaeleza kuwa, ili kukabiliana na hali ya mabadiliko ya
tabianchi yasiathiri Hifadhi hizo, juhudi za haraka zinahitajika
kuchukuliwa ikiwemo wasimamizi na wananchi wanaozunguka hifadhi kupewa
elimu ya kutosha pamoja na mipango kazi ya mara kwa mara.
Bwana Ruombano Mnege (56) mkazi wa kijiji cha Msolwa katika eneo jirani
na hifadhi ya Udzungwa anaeleza kuwa, afahamu maana ya mabadiliko ya
tabianchi, ila anachoelewa ni kuwa mambo yanabadilika pindi Mungu anapoamua.
"Mimi natambua Mungu anapoamua ndio mambo
yanatokea. Suala la mabadiliko ya tabianchi kwa sie wa huku hasa wakulima
hatutambui sana kwa sababu hatuna elimu ya kutosha” alibainisha Mnege akijibu maswali endapo wasimamizi wa hifadhi hizo
kama wanawashirikisha wananchi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Hata hivyo, wakazi wengi wa maeneo ya jirani na hifadhi wanabainisha
kuwa, hawana elimu ya kutosha katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,
hali inayowapa hofu kukumbwa na janga hilo la ukame siku za usoni.
Ambapo walibainisha kuwa, wapo watu wasio waaminifu wakiingia katika
hifadhi hizo na kukata miti pamoja na kuharibu vyanzo vya maji, kuchoma
moto misitu pamoja na kuwinda wanyama.
"Kulikuwa na wanyama wakifika hadi kwenye mashamba yetu miaka ya
nyuma. Lakini kwa sasa wanyama wale hawafiki kabisa kutokana na hali ilivyo
huenda wamepotea” anaeleza Bi. Jonesia Simon mkazi wa Sanje ambapo
anasema kutoonekana kwa wanyama hao kwa hivi sasa kumechangiwa na mabadiliko ya
tabianchi kwani kulikuwa na wanyama waliokuwa wakifuata maji na
wengine walikuwa wakifuata vyakula kwenye mashamba hayo lakini kwa sasa
wametoweka kabisa.
Mwandishi wa makala haya,
Andrew Chale wa modewjiblog.com akiwa katika eneo la
Sanje wakati wa kupanda mlima Udzungwa kuelekea kwenye maporoko ya Udzungwa
(Picha na modewjiblog team).
ramani inayoonyesha hifadhi hiyo ya Udzungwa..
Milima ya udzungwa ni jina la hifadhi inayopatikana hifadhi hiyo ndani ya
Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro pamoja na upande wa Iringa. Milima
hii ni makazi ya wanyama pori wa aina mbalimbali huku ikiwa na ukubwa wa
kilometa 1990.
Udzungwa ni miongoni mwa hifadhi zenye hazina ya aina nyingi za mimea,
ndege na wanyama ambao hawapatikani katika sehemu nyingine duniani.
Hifadhi iko umbali wa kilometa 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilometa 65
kutoka katika Hifadhi ya Mikumi ambayo ni ya jirani kabisa.
Kati ya aina sita za jamii ya nyani wanaopatikana katika hifadhi hii,
mbili hupatikana katika hifadhi hii pekee ambao ni : Mbega Mwekundu, wa Iringa
(Iringa red colobus monkey) na aina ya pili ni Sanje Crested mangabey.
Huku kukiwa na aina mbalimbali za ndege na aina nne za ndege ambao
hazikufahamika hadi katika miaka ya karibuni. Ndege ni Chozi bawa jekundu
(rufous-winged sunbrid) na wengine wengi akiwemo kwale Udzungwa.
Hifadhi hii pia ni moja ya makazi makuu na muhimu ya ndege pori barani
Afrika.
Picha ya juu Maporoko
hayo na chini ni Mwandishi wa makala haya wa modewjiblog.com, Andrew Chale akiwa
kwenye maporomoko hayo ya Udzungwa wakati alipotembelea kuandika habari
za Mabadiliko ya Tabianchi namna yanavyoweza kuathiri Hifadhi za Taifa nchini.
(Picha na modewjiblog team).
Mwandishi
wa makala haya wa modewjiblog.com,
Andrew Chale akiwa katika eneo la awali na mapumziko baada ya safari ndefu ya
kupanda mlima huo katika kuelekea kwenye maporomoko hayo ya Udzungwa (Picha na
modewjiblog team).
Maporomoko
ya Sanje:
Ndani
ya hifadhi hii pia ina Mto Sanje ambao ni kivutio kikubwa sana. Mto huu
una maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka kupitia
msituni na kututa mithili ya mianzo ya ukungu bondeni.
Hata
hivyo, mbali na kuwa na vitu vyote hivyo ndani ya hifadhi hii ya Udzungwa,
Serikali na jamii inayozunguka hiafdhi hii inawajibu mpana wa kukabiriana na
mabadiliko ya tabianchi kwani wasipochukua hatua vitu hivyo vinaweza
kutoweka na nchi ikaja kukosa mapato kwani Utalii ni miongoni mwa sekta
inayoiingizia Tanzania fedha nyingi za kimaendeleo.
Wanyama
kutoweka:
Tovuti
ya Serikali ya Makamu wa Rais (http://www.vpo.go.tz/news), imebainisha kuwa: Inakadiriwa kwamba
asilimia 34 ya ardhi ya Bara la Afrika iko katika hatari ya kugeuka
jangwa kutokana na mabadiliko ya TabiaNchi.
Na
kuongeza kuwa: Hali hii ya mabadiliko ya TabiaNchi itachangia kutoweka
kwa asilimia kati ya 25 hadi 40 ya aina fulani za wanyama katika
hifadhi Barani Afrika ifikapo mwaka 2020 na kwamba maeneo kame
yataongezeka kwa asilimia 5 hadi 8 Barani Afrika ifikapo mwaka
2080.
Msemaji wa TANAPA:
Hata
hivyo suala la mabadiliko ya tabianchi katika hifadhi za Taifa nchini bado
halijapewa kipaumbele kikubwa hasa kwa wadau wa mabadiliko ya tabianchi ikiwemo
wanahabari, wanaharakati wa mazingira na wananchi wanaoishi jirani na
hifadhi.
Hii
inatokana na hata wakati mwingine kukosa ushirikiano wa karibu kutoka kwa
mamlaka husika ikiwemo makao makuu ya ofisi za TANAPA ambao ndio wenye jukumu
la kutoa taarifa za kina kitaalamu.
Taswira ya eneo la
maporomoko ya Udzungwa inavyoonekana unapokuwa katika eneo la awali la View
Point ndani ya Hifadhi hiyo ya Udzungwa. Katika taswira hiyo panaonekana kama
ramani ya Afrika. (Picha na Andrew Chale,modewjiblog).
Eneo la maji yanayotoka
kwenye maporomoko hayo ambapo kwa kipindi hiki yanapoonekana yakiwa yamepungua
kutokana na kipindi maalum. Hata hivyo maji hayo kuna msimu yanajaa zaidi ..
Miongoni mwa aina za ndege wanaopatikana
ndani ya hifadhi hizo za Udzungwa ambapo inaelezwa kuwa Hifadhi hiyo imekuwa
ikitembelewa na ndege mbalimbali kutoka maeneo mengi ya nchi za Afrika.
Miongoni mwa miti inayopatikana ndani ya
misitu hiyo ya Hifadhi ya Udzungwa..
Miongoni mwa miti inayopatikana ndani ya
Hifadhi hiyo ambayo hata hivyo bado inakabiriwa na changamoto kwa watu wasio na
mapenzi mema kuvamia na kukata miti hiyo ya hifadhi kwa ajili ya shughuli za
mbao na mambo mengine.
Miongoni mwa miti ambayo inapatikana
ndani ya hifadhi hiyo ambayo ni dawa na pia ni miongoni mwa miti inayopendwa na
wanyama hata hivyo ipo katika changamoto ya kutoweka...
Red Col wanaopatikana ndani ya Misiti
hiyo ya Hifadhi ya Udzungwa..
Mwandishi wa makala haya wa modewjiblo,
Andrew Chale akiwa katikati ya Hifadhi hiyo wakati wa kuyatafuta Maporomoko
hayo. Ambapo ndani ya msitu huo wenye baridi muda wote kutokana na kuzungukwa
na miti mbalimbali.
Misitu hiyo ya Udzungwa inavyoonekana..
Itaendelea ripoti sehemu ya Pili…
Ripoti hii imeandaliwa na Andrew Chale, Mwandishi wa Habari na Mhariri wa
mtandao (blog) ya modewjiblog.com
ya nchini Tanzania. ( Anuani : +255719076376 au barua pepe: andrewchale@gmail.com).
Makala
haya yamefadhiliwa na kwa ufadhili wa Shirika la ( CFI) la nchini
Ufaransa, chini ya mradi wa Medias 21 Africa & Asia.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment