UTAFITI :-Soma Matokeo ya Maoni ya Wananchi kuhusu Siasa 2015 kutoka TWAWEZA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 22, 2015

UTAFITI :-Soma Matokeo ya Maoni ya Wananchi kuhusu Siasa 2015 kutoka TWAWEZA.


Utafiti huo wa taasisi ya TWAWEZA uliotokana na kuhoji watu 1848 kutoka mikoa tofauti ya Tanzania bara, inasema iliwauliza wananchi hao 1848 swali hili: Ukimwacha Rais Kikwete, iwapo uchaguzi wa urais ungefanyika leo, ungemchagua nani? ...Majibu ya swali hilo TWAWEZA wanasema limejibiwa na wananchi hao kama ifuatavyo:-


Magufuli 65 %

Lowassa 25%

Mwingine 3%

Sijui/kataa jibu 7%

Aidha, walipoulizwa watawachagua wagombea wa chama gani – bila kutajiwa majina ya wagombea – wananchi 6 kati ya 10 walisema kwamba watawachagua wagombea wa CCM kwa Urais (66%), Ubunge (60%) na Udiwani (60%). Takwimu hizi zinatoa picha kwamba CCM inaungwa mkono, kama ilivyokuwa mwaka 2012.


Takwimu zinaonyesha kwamba wananchi hawaelewi nafasi rasmi ya Ukawa

Chadema ni chama cha pili kinachopendwa kushinda vyama vingine vya upinzani. Lakini wananchi wanaosema kwamba watawachagua wagombea wa Chadema kwa Urais, Ubunge na Udiwani wamepungua kidogo. Ikumbukwe kuwa, inawezekana wananchi wanaopenda zaidi mseto wa Ukawa waliunga mkono vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi au NLD.

Mbali ya CCM na vyama vinavyounda Ukawa, chama cha ACT-Wazalendo kilitajwa na zaidi ya asilimia moja ya wananchi… Kusoma zaidi bofya HAPA.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad