Baadhi ya
wakimbizi kutoka nchini Burundi, wanaohifadhiwa katika kambi ya wakimbizi ya
Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wakiwapokea wakimbizi wenzao
(hawapo pichani) waliowasili jana kwa basi kwa ajili ya kuhifadhiwa katika
kambi hiyo.
|
Mkimbizi
kutoka Burundi,Philipo Nyandugulu(kushoto)
na mkewe Vanisi Nyandugulu,
wakisubiri taratibu za kupangiwa sehemu ya kuishi baada ya kuwasili
katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma,
baada ya kuwasili katika kambi hiyo jana,September 14,2015.
|
Mkimbizi kutoka Burundi, Vanisi Nyandugulu
akipanga vifaa vyake baada ya kuwasili katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu
iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma jana.
Wakimbizi kutoka Burundi wanaendela kuwasili nchini ambapo wanahifadhiwa
katika kambi ya wakimizi ya Nyarugusu.
|
Koplo Flora Peter wa Kituo cha Polisi katika kambi ya wakimbizi
ya Nyarugusu akiwa ameshikilia visu, panga na fimbo vilivyokutwa katika baadhi
ya mizigo ya wakimbizi kutoka Burundi wanaowasili katika kambi ya wakimbizi ya
Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Vifaa vya hatari kama vile visu, panga, fimbo
na mishale haviruhusiwi kumilikiwa na wakimbizi wapya wanaowasili kambini hapo,
kwa sababu za kiusalama.
|
Mkimbizi
kutoka Burundi, Nibaruja Europernce ,
akihamasisha wenzake wanaowasili katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko
wilayani Kasulu mkoani Kigoma kuhusu taratibu za kuishi kambini hapo ikiwani ni
pamoja na kutekeleza masuala muhimu ya kiafya, jana September 14,2015.
|
Mfanyakazi
wa Shirika la Maji na Usafi wa Mazingira (TWESA) linalofanya shughuli zake
katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma,
Andrea Niyitanga , Akimnawisha mikono kwa kutumia maji yaliyowekwa dawa, mkimbizi
kutoka Burundi ikiwa ni mojawapo ya mkakati wa kutoa elimu ya afya.
|
Mtoto Olivia
Nekwizera, ambaye ni mkimbizi kutoka Burundi akisaidiwa na mama yake kunawa
mikono baada ya kuwasili katika kambi ya wakimizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani
Kasulu mkoani Kigoma.
Kunawa mikono kwa maji yenye dawa ni jambo la lazima kwa
wakimbizi wapya kuonyesha umuhimu wa kuzingatia masuala ya afya na pia
kudhibiti magonjwa ya kuambukiza.
|
Watoto wa moja ya familia ya wakimbizi kutoka
Burundi wakielekezwa kuingia katika makazi yao mara baada ya kuwasili katika
kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Anayeelekeza ni mfanyakazi wa Shirika la Maji na Usafi wa Mazingira (TWESA)
linalofanya shughuli zake katika kambi hiyo.
|
Wakimbizi
kutoka Burundi wakipata maelezo ya jinsi ya kuishi katika kambi ya wakimbizi ya
Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma mara baada ya kuwasili kambini
hapo. Anayetoa maelekezo hayo ni Nayiga
Mireye wa Shirika la Maji na Usafi wa
Mazingira (TWESA) linalofanya shughuli zake kambini hapo.
(PICHA ZOTE
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment