Kutoka
kushoto ni,Mjumbe wa Chama Cha ACT Wazalendo,Emmanuel Mvula, Mwenyekiti wa
Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa, Nixon Tugara na Mkurugenzi wa Kampeni za
uchaguzi Taifa, Venance Msebo.
|
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa, Nixon Tugara (katikati) akisoma taarifa
yake.
|
Wanahabari
wakichukua tukio.
CHAMA cha
Act- Wazalendo hii leo kimezungumzia utafiti uliofanywa na taasisi ya Twaweza
juu ya mgombea urais kupitia chama hicho, Anna Mghwila uliotolewa jana na
viongozi wa taasisi hiyo.
Akizungumza
na wanahabari leo kwenye Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, Kijitonyama
jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa, Nixon
Tugara amesema kuwa chama cha ACT Wazalendo kimeyapokea matokeo hayo ya awali
na kuyapitia kwa kina juu ya tafiti na maoni ya wananchi kuhusu siasa uliofanywa
na taasisi ya Twaweza.
Amesema kuwa
licha ya kuonesha hali hiyo ya utafiti wao wamefarijika kwamba chama chao ni
chama pekee nje ya CCM na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA
kilichotajwa na wapiga kura zaidi ya asilimia moja, hivyo ikidai chama chao
kimekuwa cha nne katika kukubalika kwa wapiga kura nyuma ya vyama vingine.
Aliongeza
kuwa wanazidi kufarijika kwamba watafiti wamekiri wazi kuwa takwimu za utafiti
zilikusanywa katika kipindi ambacho chama chao cha ACT Wazalendo kilikuwa hakijamtangaza
mgombea wake wa urais na pia wakati huo walikuwa bado hawajatangaza wagombea
wao kupitia ubunge wala kuzindua kampeni.
Aidha
aliongeza kutokana na kufanya vizuri katika uzinduzi wa kampeni zao na bidii
kubwa ambayo mgombea wao mama Anna Mghwira na wagombea wa ubunge na udiwani
wamekuwa wakifanya katika kampeni zinazoendelea nchi nzima, hivyo ni imani yao
kama utafiti ungefanyika leo kuwa wangefanya vizuri zaidi.
”Ninachowaomba
wagombea wetu na wanachama, wapenzi wa ACT Wazalendo pamoja na viongozi wa
chama wachukulie matokeo haya ya utafiti kama changamoto ya kuongeza bidii
katika kampeni zetu,” alisema Tugara.
(NA DENIS
MTIMA/GPL)
|
No comments:
Post a Comment